.

KINANA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA KIMOMUNISTI CHA CHINA

Nov 29, 2016

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya Mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (Wakwanza kushoto),  alipokutana naye na kufanya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. Wapili ni Kaimu Balozi wa China hapa Nchini, Gou hao Domg. Na walioketi kulia, ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Katibu wa NEC, Sisa na Ushorikiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chama.

 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akimsalimia  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo kabla ya kuanza mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Kaimu Nalozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, alipowasili katika ukumbi wa Sekretarieti kwa ajili ya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo (katikati)
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akijiandaa kukaa tayari kwa mazungumzo na Jia Bo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alipowasili ukumbini. Madabida ndiye Mwenyeji wa ujumbe huo wa China


 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo ya mafunzo katika Chuo Cha Viongozi waandamizi cha Chama Cha Kikomunisti cha China, Jia Bo katika picha ya pamoja na ujumbe wa CCM na CPC, baada ya mazungumzo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salam. Bo na ujumbe wake wapo katika ziara ya mafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Mapinduzi. 
 KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman akiagana na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Gou Hao Dong, baada ya mazungumzo.
Balozi wa China hapa nchini, Gou Ho Dong akiagana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana baada ya mazungumzo hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, ramadhani Madabida. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª