Uchunguzi mpya wa maoni unaonyesha kuwa,
zaidi ya asilimia 80 ya Wamarekani wanaamini kuwa, nchi hiyo imekumbwa
na mpasuko mkubwa baada ya uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni.
Televisheni ya CNN imetangaza kuwa, uchunguzi wa maoni
uliofanywa na taasisi ya Auarsy unaonyesha kuwa, asilimia 85 ya raia wa
Marekani wanaamini kuwa mpasuko na tofauti juu ya masuala muhimu
vimeshadidi zaidi mwaka huu nchini humo ikilinganishwa na miaka
iliyopita.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, Wamarekani wengi wanapinga vikali mfumo
wa demokrasia inayotawala hivi sasa nchi humo hasa baada ya uchaguzi wa
rais uliompa ushindi Donald Trump wa chama cha Republican. Asilimia
kubwa ya raia wa Marekani walimpigia kura Hillary Clinton katika
uchaguzi wa tarehe 8 Novemba mwaka huu lakini Tume ya Uchaguzi ya nchi
hiyo ilimtangaza Trump kuwa mshindi. Hii ni baada ya mgombea huyo wa
chama cha Republican kupigiwa kura 290 kati ya 538 za wawakilishi wa
majimbo 50 ya nchi hiyo, huku Clinton akipata kura 228 pekee.
Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni yanaonesha kwamba, idadi kubwa ya
raia wa Marekani wanasisitiza udharura wa kufanyiwa marekebisho katiba
ya nchi hiyo ili kuruhusu rais achaguliwe na wananchi peke na si
vinginevyo.
Wiki iliyopita pia taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Gallup ilitoa
matokeo mapya ya uchunguzi wa maoni yaliyoonyesha kwamba, raia wengi wa
Marekani wanaamini kuwa, mpasuko umezidi kuongezeka nchini humo kuliko
kipindi kingine chochote. Wamarekani wengi wanataka kuheshimiwa uamuzi
wao na kumtangaza Hillary Clinton kuwa mshindi badala ya Trump.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269