Breaking News

Your Ad Spot

Nov 29, 2016

UN NA EU ZALAANI SHAMBULIZI LA KIGAIDI KATIKA SOKO NCHINI SOMALIA

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya zimelaani shambulizi la kigaidi lililotokea katika soko la mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Taarifa iliyotolewa na Michael Keating, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia imelaani vikali shambulizi lililolilenga soko la mji Mogadishu na imewataka askari wa serikali kuwabaini wahusika wa hujuma hiyo na kuwafikisha mahakamani.
Umoja wa Ulaya pia imelaani hujuma hiyo iliyoua raia kadhaa mjini Mogadishu na  kutangaza azma yake ya kufanya juhudi kubwa kwa ajili ya kudhamini usalama wa taifa hilo la Pembe ya Afrika.
Sehemu ya hujuma za magaidi Somalia
Mripuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari uliotokea Jumamosi iliyopita katika lango la kuingilia soko la mji mkuu wa Somalia, Mogadishu uliua zaidi ya raia 10 wengi wao wakiwa wanawake. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na hujuma hiyo, ingawa kundi la kigaidi na kitakfiri la ash-Shabab limehusishwa na jinai hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages