Breaking News

Your Ad Spot

Nov 27, 2016

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA KAMPALA JIJINI DAR ES SALAM

 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.

Mahafali yakiendelea


Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

Na Mwandishi Wetu
RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.

Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.

Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika 
maisha yao. 

"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele 
yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.

Aidha Rais huyo mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili 
kuweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla. 

Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo kupitia 
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB). 

Akihimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili
kuchochea matumizi yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China, Urusi, USA, Iran na mengineyo.

Alisema Afrika lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha pekee inayozungumzwa na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna kila sababu ya kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi katika mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na salamu zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.

Awali akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika fani mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages