.

ZIARA YA MAKONDA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI WILAYA YA KINONDONI YANOGA LEO, AKATIZA VICHOCHORO KUSAKA KERO, ACHAPA KAZI KIKAMILIFU NA AFANDE SIRRO, AMTUMBUA MGANGA MKUU

Nov 27, 2016

 TUCHAPE KAZI KIONGOZI: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimwaga kicheko na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya mkoa huo, walipokuwa wkijadili jambo, baada ya kuzungumza na viongozi na watendaji kutoka wilaya ya Kinondoni, katika Bwalo na Maofisa wa Polisi, Msaki mwanzoni mwa ziara yake katika mkoa wa Dar es Salaam, leo. Zifuatazo ni taswira katika picha kama alivyowanasa Mmiliki wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo aliyekuwa katika ziara hiyo.  
 TANDALE
­čö╗
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikagua chumba cha biashara cha Mamalishe (kushoto), aliyemkuta akiwa kazini eneo la Tandale, akiwa katika ziara ya kusikiliza kero za wananchi
Makonda akimwangalia mamalishe huyo wakati akiandaa chakula 
 Makonda na msafara wake wakikatiza mitaa ya Tandale wakati akisaka kero za wananchi wakati wa ziara hiyo ya aina yake. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wanne ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.
 Salum Ali Hapi akimpa maelezo Makonda walipofika kukagua eneo maarufu kwa jina la Uwanja wa Fisi, lililopo Tandale, Kata ya Manzese
 Makonda akizungumza na wateja wa pombe za kieyeji aliowakuta katika kwenye kilabu cha pombe hizo, eneo la Uwanja wa Fisi
Jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Mandela akikata funda la pombe ya kienyeji mbele ya Makonda bila wasiwasi kuwa yupo na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  
 Makonda akijaribu kupiga hodi kwenye moja vya vyumba inayoelezwa kuwa ni ya madanguro ya ukahaba katika eneo hilo la Uwanja wa Fisi. Pamoja naye ni Hapi na Sirro 
 Kamanda Sirro naye akijaribu kumsaidia Makonda kupisha hodi lakini pia bila mafanikio ya kuitikiwa na waliokuwa wamejifungia ndani 
 Makonda akichukua bia kutoka kwa mhudumu wa baa pekee aliyoikuta wazi wakati myinge zote zikiwa zimefungwa kuhofia ujio wake.
 Makonda akiitazama kwa makini bia hiyo kuona tarehe yake ya mwisho wa matumizi, ili kujiridhisha kwa kuwa huelezwa kwamba baa zilizopo eneo hilo la Uwanja wa Fisi huuza vinywaji hadi vilivyokwisha mda wake wa matumizi. Bia hiyo aliikuta bado inafaa kwa matumizi.


 SHULE
 Makonda akitazama paa la chumba cha darasa katika shule ya Msingi Tandale, lililoporomoka wakati wa upepo mkali ulioambatana na mvua


MIUNDOMBINU YA BARABARA
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akitazama majitaka yakitiririka kwenye daraja la barabara kutoka Tandale kwenda Mwananyamala. Makonda aliahidi barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami, la kwamba kabla ya hatua hiyo itafanyiwa matengenezo ya awali kuziba makorogoro ili iweze kupitika. 
 Makonda akipita pembeni pembeni kukwema maji machafu yaliyotuama kwenye sehemu ya barabara hiyo
 Mara huyu mama naye akamvaa na kumweleza kero zake wakati akipita

MKUTANO UWANJA WA SHULE YA MSINGI TANDALE
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Salum Ali Hapi akimkaribisha Makonda kuanza kuunguruma ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu papo hapo au baadae, katika mkutano wa hadhara uliofayika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Tandale, leo
 Makonda akizungumza 
 Makonda akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.
 Umati wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akifuatilia jambo kwenye simu yake wakati wa mkutano huo. Mpogolo ni miongoni mwa waratibu wa ziara hiyo ya siku kumi ya Makonda katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam.
 Watu wa huduma ya kwanza wakimpeleka kwenye gari ili kupelekwa haraka hospitali baada ya kuangua wakati wa mkutano huo
 Akiingizwa kwenye gari la wagonjwa la Manispaa ya Kinondoni
 Wananchi kwenye mkutano huo
 Makonda akianza kujibu kero kwa kuwahoji watendaji kulingana na wananchi walivyotaka kujibiwa kero husika.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni, Azizi Msuya (aliyeshika kinasa sauti), akisubiri hukumu ya Makonda baada ya kushindwa kueleza ikiwa alikuwa anajua au hajui kadhia ya dawa kuibwa mara kwa mara katika Zahanati ya Tandale kama wananchi walivyolalamika, ambapo alisema hajui
" Haiwezekani uwe Mganga Mkuu wa Wilaya katika mkoa wangu halafu hujui kuhusu kuibwa kwa dawa kwenye zahanati, hii haikubaliki, kuanzia sasa si mganga Mkuu wa Kinondoni, Nitawaambia wizara inayokuhusu wakupangine wilaya katika mikoa mingine ambako watavumilia uzembe kama papo", alisema Makonda wakati akimtumbua Msuya kwenye mkutano huo wa hadhara uliofanyika shule ya Msingi Tandale. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- theNkoromo Blog

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª