.

WAHAJIRA 550 WAAFRIKA WAOKOLEWA BAHARI YA MEDITERANNEA WAKIKIMBILIA ULAYA

Nov 15, 2016

Wahajiri 550, aghalabu kutoka Afrika Magharibi, wameokolewa kutoka katika boti zao zilizokuwa zinaelekea kuzama katika Bahari ya Mediterranea Jumatatu katika oparesheni tano ambapo waokoaji walipata miili mitano.
Gadi ya Pwani ya Italia iliyotekeleza oparesheni hiyo inasema wahamiaji hao haramu walikuwa  wakisafiria katika boti ndogo  za plastiki wakati waokoaji walipowaona wakizama.
Kati ya walionusuriwa ni mvulana ambaye alikuwa amezimia kwa masaa mawili na mwanamke ambaye alikuwa amekunywa mafuta ya petroli kimakosa.
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linasema hadi sasa wahajiri 159,496 wamefika katika pwani ya Italia kwa boti ambapo 4,271 wengine wamepoteza maisha wakijaribu kuingia Ulaya kwa njia hiyo ya Bahari ya Mediterranean.
Wahajiri haramu
Njia hatari zaidi inayotumiwa na wahamiaji haramu kuingia Ulaya kupitia Bahari ya Mediterenea ni ile ya Libya kuelekea Italia ambapo wasafirishaji binadamu wanatumia fursa ya kukosekana usalama katika nchi hiyo kuwapakia watu katika boti zisizoweza kutumika baharini.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช