Wahajiri 1,400 aghalabu kutoka kaskazini mwa
Afrika, wameokolewa baada ya boti zao kuzama katika Bahari ya
Mediterranea wakielekea barani Ulaya.
Gadi ya Pwani ya Italia iliyotekeleza operesheni hiyo ya jana
Jumanne imesema wahamiaji hao haramu ambao safari yao ilianzia nchini
Libya walikuwa wakisafiri katika boti ndogo za plastiki zipatazo 11
wakati waokoaji walipowaona wakizama na kwamba miili minane imepatika
katika operesheni hiyo ya uokoaji.
Wapiga mbizi hao wa Italia wamesema watatu kati ya manusura wa ajali
hiyo wapo katika hali mbaya na kwamba wanahitaji huduma za dharura za
matibabu.
Haya yanajiri siku chache baada ya wahajiri wengine wapatao 550,
akthari yao wakitokea Afrika Magharibi, kuokolewa kutoka katika Bahari
ya Mediterranea wakielekea Italia.
Hii ni katika hali ambayo, Shirika la Kimataifa la Wahamiaji
limetangaza kuwa, kiiwango cha maafa ya wahajiri baharini kimeongezeka
mara sita mwezi huu wa Novemba ikilinganishwa na mwezi kama huu mwaka
jana.
Shirika hili hivi karibuni lilisema kuwa, idadi ya wahajiri
waliopoteza maisha yao katika Bahari ya Mediterranean imepindukia watu
4,636. Kwa mujibu wa takwimu rasmi za shirika hilo, tangu mwanzoni mwa
mwaka huu 2016, karibu wahajiri laki tatu na 43 elfu na 589 wameingia
barani Ulaya kwa njia ya baharini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269