Breaking News

Your Ad Spot

Nov 30, 2016

WAHITIMU 57 WA ELIMU YA ANGA WATUNUKIWA VYETI MKOANI KIGOMA

NA RIPOTA  MAGRETH MAGOSSO MKOANI KIGOMA
ZAIDI ya wahitimu 50 kutoka Chuo Cha Hali ya Hewa  kilichopo wilaya ya kigoma Mkoa wa Kigoma,wameaswa  wafanye kazi kwa kuzingatia weledi,maadili na taratibu za watumishi wa umma,ili  kutoa huduma bora kwa maendeleo ya  Taifa.

Hayo yalibainika jana kigoma ujiji,kwenye mahafali ya 14  ya utoaji wav yeti kwa wahitimu  33 wa ngazi ya cheti  na mahafali ya tano  kwa wahitimu 24  ngazi ya  Stashahada waliohitimu elimu ya Anga ambapo ikitumika  sahihi  taifa litajihami na majanga mbalimbali hasa mabadiliko ya tabia nchi.

Akifafanua hilo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Laurent  Shauri alisema wahitimu hao wamepewa mafunzo stahiki ya watumishi wa umma  ambayo yanalenga maadili,weledi,taratibu na miongozo ya kazi ili,kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya taifa na waepuke  ngono zembe  inayopelekea  janga la ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini(UKIMWI).

Pia, chuo kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa bweni za wanafunzi na miundombinu bora ya utoaji wa elimu hiyo ambayo ni muhimu katika kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi na kutoa fursa kwa wakulima kutumia utabiri huo ili kulima kilimo chenye tija utakaonufaisha sektan hiyo.

Akifunga sherehe hizo Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa  Emanuel Maganga alisema  taaluma yao ni chachu ya kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi,magonjwa na kuinua sekta ya kilimo na kuisihi mamlaka ya hali ya hewa iongeze vifaa vya kisasa ili kutabiri  ukweli itakuwa na thamani kwa jamii endapo utabiri  utakuwa wa kweli.

Mmoja wa wahitimu  hao Praseda Rafaeli alisema  atafanya kazi kwa uaminifu mkubwa kwa mujibu wa miongozo  ya taaluma yao ambayo ni tija kwa taifa kukabiliana na mafuriko,ukame ambapo utabiri wa kweli ni pamoja na vifaa vya kisasa ambavyo vitawapa mwelekeo na dira ya hali halisi ya hewa na namna ya kukabiliana na matukio yajayo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages