SERIKALI
kupitia kitengo maalum cha uchunguzi wa jinai ya kimtandao, imefanikiwa
kukamata watuhumiwa 690 kwa tuhuma za kufanya uhalifu wa mtandao.
Watuhumiwa
hao ni matapeli, wezi, waporaji wa simu za mkononi na wengineo
wanaotumia mfumo wa intaneti kuibia watu wasiokuwa na hatia.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projestus Rwegasira
alisema juzi jioni kuwa ofisi yake imekuwa ikikabiliana kikamilifu na
wahalifu hao.
Alisitiza
kwamba wahusika wote wa vitendo hivyo, watakamatwa. Meja Jenerali
Rwegasira alikuwa akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha
Tunatekeleza, kinachorushwa na Televisheni ya Taifa(TBC). Kwamba wizara
yake kwa kushirikiana na vyombo vya serikali, inaandaa mashtaka dhidi ya
watuhumiwa waliokamatwa na watafikishwa mahakamani.
“Tunafanya
kila juhudi kuzuia vitendo vya uhalifu wa kimtandao, tayari tumekamata
baadhi ya watuhumiwa na watakabiliana na mkono wa sheria mahakamani,”
alisema.
Alisema
serikali imeunda kitengo maalumu chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani,
kukabiliana na udanganyifu na uhalifu wa kimtandao nchini na kimekuwa
kikifanya kazi nzuri.
Rwegasira
alisema, “Ningependa kuutangazia umma kuwa huru kutoa taarifa ya
vitendo kama hivyo polisi mara wanapoona, tuna uwezo wa kufuatilia simu
zilizoibwa na kuwakamata watuhumiwa”.
Mwezi
Januari mwaka huu, Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Veronica Sudayi alisema tangu kupitishwa kwa
Sheria ya Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki ya 2015 mwezi
Septemba 2015, kiwango cha wizi na udanganyifu nchini, kimepungua kwa
asilimia 60.
Sudayi
alisema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa Taasisi
ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kuhusu Sheria hiyo ya Makosa ya
Mtandao. Kuhusu amani na usalama, katibu mkuu huyo alisema serikali
imejiandaa vya kutosha kulinda watu na mali zao na kujipanga vya
kutosha.
Alisema
jeshi la polisi liliweza kukabiliana na changamoto za kiusalama katika
mikoa ya Tanga na Mwanza baada ya watu wasiokuwa na hatia kuuawa na
majambazi. Alisema katika tukio la Tanga, watuhumiwa 28 walikamatwa na
wengine nane walikamatwa kuhusiana na tukio la Mwanza.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269