Kituo cha habari cha Magharibi cha Global
Reserach kimefichua katika ripoti yake mpya majina ya waungaji mkono wa
kimataifa wa makundi ya kigaidi.
Global Reserach imeeleza kupitia taarifa yake kuwa nchi sita
ikiwemo Saudi Arabia, Uturuki, Qatar, Uingereza, Ufaransa na Marekani
pamoja na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio waungaji mkono
wakuu wa makundi ya kigaidi duniani likiwemo la Daesh.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwaka 2006 Saudia ilipokea agizo la moja
kwa moja la Marekani kuitaka iunde kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq
ili kuzuia nchi hiyo isiwe na uhusiano wa karibu na Iran.
Mnamo mwaka 2011 Saudi Arabia ilitoa msukumo kwa harakati za utumiaji
silaha katika mji wa Dar'a kusini mwa Syria na kuyasaidia kwa fedha na
silaha makundi yote ya wabeba silaha nchini humo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Global Reserach Uturuki nayo imekuwa
ikitumika kama kivuko salama kwa makundi ya wabeba silaha yanayoelekea
kaskazini mwa Syria; na kwa kushirikiana na Saudia imeunda kundi la
kigaidi la Jabhatu-Nusrah (Fat-hu Sham). Vilevile katika miaka ya
karibuni, serikali ya Ankara imefungua mipaka ya nchi hiyo kwa ajili ya
makundi ya kigaidi yanayoelekea nchini Syria.
Global Research imeendelea kufichua kupitia ripoti yake kuwa mwaka
2013, Qatar ilisaidia na kuunga mkono uundaji wa genge la kigaidi
liitwalo Jaishul-Fat-h uliosimamiwa kwa pamoja na Saudi Arabia na
Uturuki.
Uingereza nayo iliyasaidia kwa silaha makundi ya wabeba silaha nchini
Syria kwa madhumuni ya kushirikiana kwa karibu na vikundi vidogo vidogo
vya mtandao wa Al-Qaeda. Nayo serikali ya Ufaransa imekuwa ikifuata
sera sawa na Uingereza katika kuyasaidia kwa silaha makundi yanayobeba
silaha nchini Syria.
Utawala wa Kizayuni wa Israel umetajwa katika orodha ya Global
Research kuwa mtoaji misaada ya zana na silaha za kivita pamoja na
huduma za tiba kwa wabeba silaha wote nchini Syria. Daesh na
Jabhatu-Nusrah ni miongoni mwa makundi ya kigaidi yanayopewa misaada na
kuungwa mkono na utawala wa Kizayuni.
Nafasi ya Marekani katika kuliunga mkono kundi la kigaidi na
kitakfiri la Daesh imetajwa na Global Reserach kuwa kubwa na pana zaidi
kwa kusaidia harakati zote za kundi hilo katika eneo la Mashariki ya
Kati.../
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269