Breaking News

Your Ad Spot

Dec 6, 2016

MAKOMANDOO KUPAMBA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 55 YA UHRU

Na: Frank Shija – MAELEZO
MAKOMANDOO wa Jeshi la Ulinzi wanatarajiwa kupamba sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo wwatacheza  gwaride  la kimyakimya.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Jenista amesema kuwa mbali na maonyesho hayo pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya Bendi ya Muziki wa kizazi kipya na Kizazi cha zamani, ngoma za asili za mikoa ya Mbeya, Pwani, Lindi na kimoja kutoka Zanzibar.
Waziri Mhagama ameongeza kuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Uhuru siku hiyo ya tarehe 9 Desemba ili kusjumuika na Watanzania wote katika kuadhimisha sherehe hizo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu”  (P.T)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages