Rais Obama ameamuru kutimuliwa
kwa wanadiplomaisa thelathini na tano wa Urusi kufuatia tuhuma za Urusi
kutaka kuingilia kati uchaguzi wa Marekani kupitia njia ya mtandao.
Makazi ya wanadiplomasia wawili wa Urusi yamefungwa na baadae kuwekewa vikwazo.
Rais Obama amesema Urusi imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani na ametahadharisha hatua zaidi kuchukuliwa.
Obama ameendelea kusema wamarekani wote sharti washtushwe na vitendo
vya Urusi, hii ikionekana kama njia ya kumjibu mrithi wake Donald Trump
ambae amesema kila mtu aishi maisha yake.
Kwa upande wake, rais
mteule mara kwa mara amekuwa akizipuuzia taarifa hizo za udukuzi, lakini
hivi amesema atakutana na wakuu wa mashushu wa Marekani ili kulijadili
hilo.
Urusi nayo imekana tuhuma za kufanya udukuzi mfumo wa mtandao wa chama cha Democratic.
Msemaji wa serikali ya Urusi amesema Urusi nayo italipiza kwa kiwango hicho hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269