.

PEMBE ZA FARU JOHN ZAWASILISHWA KWA WAZIRI MKUU MAJALIWA

Dec 9, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa pembe za faru John na Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori,(Acting  Assistant Director of Anti-poaching, Wildlife Division), Bw. Robert Mande, (kulia) wakati wa kikao kilichofanyika kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Hatua hiyo inafuatia agizo alilolitoa Waziri Mkuu wakati akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Ngorongoro, kuwa wawasilishe vielelezo vyote vya namna gani na kwanini Faru John alihamishwa kutoka makazi yake hapo Ngorongoro na kupelekwa kwenye hoteli moja ya kitalii na hatimaye kudaiwa kufa. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyeshwa pembe za faru John na  Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangiri wa Wanyamapori  (Acting Assistant Director of Antipoarching, Wildlife Division), Bw. Robert Mande, katika kikao kilichofanyika kwenye Makazi yake jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne maghembe.


Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangiri wa Wanyamapori  (Acting Assistant Director of Antipoarching, Wildlife Division), na Bw. Robert Mande (kulia) na Mkuu wa Hifadhi ya Ikorongo Gurunetya Serengeti, Nollosco Ngowe wakiwa wamebeba sanduku lenye pembe za faru John baada ya kumwonyesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 9, 2016

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª