.

RAIS MAGUFULI: SHEREHE ZA UHURU LEO MWISHO KUFANYIKA DAR, MWAKANI KUFANYIKA DODOMA

Dec 9, 2016

Na Bashir Nkoromo, Dar
Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amehitimisha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika, katika shamrashamra zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akihutubia katika sherehe hizo, Dk. Magufuli amesema mambo kadhaa, akitangulia kusema, kwamba sherehe za mwaka huu, huenda ndiyo zikawa za mwisho kufanyika jijini Dar es Salaam.


Dk. Magufuli amesema, badala ya kufanyika Dar es Salaam, mwakani sherehe hizo zitafanyika Dodoma ambayo ndiyo Makao Makuu ya Nchi.


Amewataka wakazi wa Dar es Salaam, wanaopenda burudani ya gwaride la Majeshi ya Ulinzi na Usalama, mwakani kusafiri kwenda Dodoma ili kuona burudani hiyo.


"Nadhani wale wakazi wa Dar es Salaam, wanaopenda burudani hii ya gwaride la majeshi yetu, mwakani watalazimika kusafiri kwenda Dodoma ili kuiona burudani hii nzuri", alisema, Rais Dk. Magufuli.


Rais Magufuli alieleza kuwa sherehe alizohudhuria leo ni za mara ya pili ingawa mwaka jana hazikufanyika kama leo.


"Najua wapo watakauliza, nasemaje hii nimehurudhuria shere ya pili wakati mwaka jana haikufanyika, lakini ukweli sherehe ilifanyika ispokuwa tuliifanya kwa kufanya shughuli za usafi",


"Niliamua hivyo kwa sababu nipouliza gharama niliambiwa ni sh. bilioni nne, nikauliza fedha hizi nikwa matumizi gani, nikaambiwa ni kwa ajili ya wageni, posho na chakula. Nikauliza je chakula hiki kitaliwa na Watanzania wote? Nikaambiwa hapana. Basi nikaamua fedha hizo zitumike kutengeneza barabara ile ya Ali Hassan Mwinyi inayoenda kule Mwenge ambayo itatumiwa na Watanzania wengi." Alisema, Rais Dk. John Magufuli na kuongeza;


"Najua wapo waliokwazika na uamuzi lakini kama wapo naomba mnisamehe, na leo baada ya sherehe hizi hapa Uwanjani tumemalizana hakuna shughuli nyingine" Alisema Rais Dk Magufuli.


Sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula na Mwenyekiti wa CUD Profesa Ibrahim Lipumba, zilishereheshwa kwa gwarige, ngoma za burudani na kwaya. >>ZAIDI BOFYA HAPA


HABARI PICHA
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 9, 2016 amewaongoza mamilioni ya watanzania kusherehekea Uhuru wa Tanzania Bara kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo kivutio kikubwa kilikuwa kikosi maalum cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Makomandoo ambapo pamoja na kuonyesha umahiri wao katika medani za kivita, lakini kubwa ni komandoo hao kulala juu ya misumari yenya ncha huku wengine wakimkanyaga mwenzao aliyelalia misumari, kifuani. Pichani Komandoo huyo akionyesha maajabu hayo. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
 Komandoo wakionyesha jinsi ya kupambana na adui bila ya kutumia silaha
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dk. John Magufuli, akikagua gwaride la vikosi vya majeshi hayo wakati wa maadhimisho hayo.
Paride la kimyamimya
 
Amiri Jeshi waMjeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru akiwa kwenye gari la wazi la Kijeshi
Amiri Jeshi waMjeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru akiwa kwenye gari la wazi la Kijeshi
 
Wakati Rais Dk Magufuli akitoa hotuba yake
 Rais Dk Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa katikati ni Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein
Rais Dk Magufuli akionyesha furaha wakati akikagua gwaride kikosi cha Brass Band
Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akimsalimia Jaji Mkuu. Katikati ni Waziri Mkuu
 
 Baadhi ya wananchi wakitazama kutokea uwanja waTaifa kilichokuwa kikiendelea kwenye uwanja wa Uhuru
 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
Rais akipigiwa mizinga na wimbo wa Taifa
Rais akiagana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Rais akisindikizwa na Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliokuwa wakitembea naye kwa miguu wakati akiondoka Uwanjani
Rais Dk Magufuli akisalimiana na Mzee Mwinyi
Rais akiwaaga wananchi baada ya sherehe
 
 

Rais Dk. John Magufuli akiagana na Mjane wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kabla ya kuondoka Uwanjani/ Hotoba ya Rais Magufuli/BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช