NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
NCHI
ya Denmark imesaidia kiasi cha Cha fedha cha Sh,milioni 47,zimetumika
katika ujenzi wa mradi wa Jengo la wafanyabiashara mbalimbali wa wilaya
ya Kakonko mkoani humu,uliolenga kutoa huduma za kitaalamu juu ya
biashara na namna ya kupata soko za bidhaa hizo.
Akithibitisha hilo Ofisa Biashara wa wilaya ya kakonko Erasmus
Kishongoli katika ukabidhiwaji wa jengo hilo kwa Mkurugenzi mtendaji wa
wilaya hiyo Lusubilo Joel Kanal alisema kwa msaada wan chi hiyo
kupitia shirika la Maendeleo ya biashara la( LIK) wamefanikiwa kujenga
jengo hilo,kwa kiasi hicho cha fedha,ambapo itawapatia uelewa
wafanyabishara juu ya shughuli zao hasa upatikanaji wa soko kwa bidhaa
zenye kiwango cha kimataifa.
Akipokea jengo hilo Mkurugenzi wa wilaya hiyo Lusubiro Joel alisema
kukamilika kwa jengo hilo ni fursa kwa wafanyabishara kupunguza gharama
za kufuata huduma za ushauri wa kibiashara mjini na wawatumie wataalamu
ili kuongeza ufanisi wa bidhaa zao na kukidhi soko kwa walaji.
Akitoa mwito kwa wafanyabishara Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Hosea Ndagala
alisema kuwa lengo la Kituo hicho ni walengwa kufanya shuguli zao
kitaalamu na usasa na kuwasihi walitumie ipasavyo mara litakapoanza
shuguli zake na watumie fursa ya ujirani mwema na wakazi waishio mpaka
mwa Nchi Jirani ya Burundi ,ili kubadilishana uzoefu.
‘’Itabidi mtumie nafasi hii kufanyabiashara na majirani zenu kwa
kuutumia vizuri mpaka huu, ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya biashara
kwakuwa kituo hik kitakuwa na mambo yote muhimu lakini hata watoa huduma
watatakiwa kuacha urasimu ambao uchangia kukwamisha wengi kusonga mbele
alisema Kanali Ndagala’’
Kwa upanmde wa wafanyabiashara Musa Marko na Hamisa Amad kwa nyakati
tofauti walisema changamoto ya elimu ya ujasiliamali ni moja ya janga la
kutolipa kodi,kwa kuwa wengi hawajui kiwango cha ulipaji kodi kulingana
na biashara hali inayochangia kufanya bishara zao gizani.
Kituo hicho kinatarajia kutoa huduma za uhamiaji usajili wa majina ya
Biashara Elimu ya ulipaji Kodi na kuwaunganisha wafanyabiashara na
Taasisi za serikali na litakuwa likitumia mfumo wa kisasa wa
kielectronic ili kurahisishahupatikanaji wa huduma .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269