.

RISASI 408 ZAKAMATWA KIGOMA NA AJITUNDIKA KISA KUACHWA

Dec 9, 2016

NA MAGRETH MAGOSSO, KIGOMA


MTU Mmoja jina lake (hifadhini ) atafikishwa mahakama ya wilaya ya Kigoma  kwa tuhuma za kukutwa na Brifkesi ikiwa na risasi 408 za bunduki aina ya SMG na SAR.
Akithibitisha Kauli hiyo juzi ofisini kwake kigoma ujiji, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui alisema Desemba,5 ,2016, saa 2.20 katika kijiji cha Makere, tarafa ya makere wilayani kasulu askari polisi wakiwa katika doria walipewa tarifa na wananchi wema juu ya mtuhumiwa huyo na ndipo wakamtia nguvuni.

“walimfikisha katika kituo cha polisi makere, walimpekua hiyo brifikesi na kukuta risasi  sanjari na nguo, vitau kukamatwa kwake ni  uthubutu wa wananchi wachache kulisaidia jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu ambao wanakiuka maadili ya taifa kwa ujumla” alifafanua Kamanda huyo.
katika tukio la pili Mwanamume mmoja aliyefahamika kwa majina ya Hussein Athuman (36) mkazi wa mwanga vamia mtaa wa Msikiti madina Manispaa ya Kigoma Ujiji wilaya ya kigoma mkoani humu, amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani baada ya kukimbiwa na mkewe.

Akifafanu hilo Kamanda Mtui alisema Desemba,6 ,mwaka huu saa 4.00 asubuhi  kaka wa marehemu Salum Hamimu alienda kumtembelea ndugu yake huyo baada ya kuelezwa na dada yao aishie mkoani Tabora kuwa usiku wa desemba,5 mwaka huu marehemu alimpigia simu dada huyo kuwa mkewe kaondoka nyumbani .

Alisema  ana siku ya Nne haonekani nyumbani  na kukiri walikuwa na ugomvi,  hivyo amweleze kakake kuwa atachukua mamuzi magumu ,ndipo siku iliyofuta kakake alienda nyumbani kwa mlengwa na alipogonga alikuta ukimya mkubwa alipotumia nguvu na kufungua mlango ndipo alikuta nduguye amejitundika darini kwa kamba ya katani.

Aidha katika msako wa wahalifu walifanikiwa kukamata wahamiaji haramu 63,  pombe ya moshi lita 224 na bhange debe 02,bila kutoa ufafanuzi wa wahalifu hao na vithibitisho hivyo pia litoa rai kwa wananchi kuwa kila mwananchi anajukumu la kutii sheria bila shuruti kutoa tarifa kwa vyombo vya usalama kwa mtu yeyote mwenye kiashiria cha uhalifu  ili sheria ichukue mkondo wake.
mwisho.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª