.

WATENDAJI WA CCM, UNGUJA NA PEMBA WATUNUKIWA VYETI VYA KUHITIMU MAFUNZO

Dec 8, 2016

Na Is-haka Omar, Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Chama kitaendelea na utamaduni wa kutoa mafunzo kwa watumishi na watendaji wake ili waweze kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa  ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya mwaka 2015/2020.

Vuai alisema hayo leo katika hafla ya kuwakabidhi vyeti watendaji wa Chama Cha Mapinduzi, Unguja na Pemba katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Sekretarieti katika Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kiswandui mjini Zanzibar.

Alisema anamamini elimu waliyoipata matendaji hao itaweza kuwasaidia kuongeza uwezo na ufanisi katika shughuli zao za kiutendaji katika ofisi zao kwa wageni wanaofika katika maofisi yao.

Vuai alieleza  mafunzo hayo yametokana na matakwa ya ibara ya 188 ya Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inayoelekeza kutolewa kwa mafunzo zaidi kwa makada na viongozi mbali mbali ili wawe na weledi mkubwa katika masuala tofauti ya Chama.

Alisema licha ya ilani ya ccm kuagiza kufufua vyuo vya uongozi na siasa vya CCM ambavyo ni ilemi na Tunguu huku wakifikiria maamuzi ya kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji hao kadri uwezo wa uendeshaji wa mafunzo utakavyoruhusu.

“ Tumieni mafunzo haya kama fursa ya kujiongeza kiutendaji ili muweze kufanya kazi zenu kwa weledi na kujiamini zaidi.”, alisema Vuai.

 Hata hivyo aliahidi kuwa mafunzo hayo yatafanyika kwa awamu mbali mbali kadri uwezo wa uendeshaji wake utakavyoruhusu ili Watumishi na watendaji waweze kupata fursa hiyo ya kitaaluma.

 Alifafanua kuwa taaluma waliyopata itawasaidia katika majukumu mbali mbali yakiwemo uchaguzi katika chama na kuwataka ifikapo mwakani watoe fomu ya uongozi kwa kila mwanachama aliyekuwa na sifa na bila ya upendeleo ili zoezi hilo likfanikiwe kwa asilimia kubwa.

Nae mshiriki  wa mafunzo mafunzo hayo katibu wa CCM wilaya ya Mkoani Pemba Abdalla Yussuf Ali alisema mafunzo hayo watafanyia kazi kama ilivyokusudiwa sambamba na kuitumia elimu waliyoipata.

Aidha alisema kuwa wataitumia elimu hiyo kwa kwa kuleta tija ya kuonekanwa kuwa ofisi zao zitakuwa ni za mfano na za kuigwa.

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja   ziliwasilishwa mada sita ambazo ni Uanzishwaji masjala na utunzaji kumbukumbu za Ofisi kwa usalama, Uendeshaji wa shughuli za Ofisi na mawasiliano ya kiofisi na Taratibu za uendeshaji wa mikutano.

Zingine ni  Dhana ya utawala bora na uzalendo katika utandawazi pamoja na Huduma kwa mteja na utunzaji wa muda, yalikuwa na washiriki 42 kutoka Pemba na Unguja.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช