Mwakilishi
wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo
la Temeke - Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga
mfumo wa maji taka inaendelea.
Na Lulu Mussa
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika
miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.
Akiwa
katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa
kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi
wa eneo hilo.
Waziri
Makamba ameugiza uongozi wa Dezo Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha
ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke
unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa
kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.
“Nataka
mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni
jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka
mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki”
Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozunguuka eneo hilo kuacha mara moja
utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na
kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa
adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
“Kwa
kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo
mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa
mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”
Pia,
Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha
Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na
uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili
kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.
“Natoa
wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka
ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
Waziri
Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -
NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa
Gereji bubu zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya
shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.
Ujenzi wa
Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka
katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu
wa Rais kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na
unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi
huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.
Waziri
Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa
Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la
Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akiongea na Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe. Adam Fugame
(katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa
maji taka katika eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam
Sehemu ya
Mfereji wa Maji taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya
Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na
unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba akiongea na Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya
kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka
kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais –
Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya ziara ya
kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais. Kulia ni Bw. Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa
Mradi na Bw. Richard Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269