Breaking News

Your Ad Spot

Jan 2, 2017

MTENGA -VYAMA PINZANI ACHENI POROJO AVITAKA KUONGEA KWA DATA/TATHMINI

 Diwani wa viti maalum,Kibaha Mjini Selina Wilson akimwombea kura mgombea mteule kupitia CCM kata ya Misugusugu katika uzinduzi wa uchaguzi mdogo katika kata hiyo
 Katibu wa CCM mkoani Pwani,Hassan Mtenga akizungumza jambo katika kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Misugusugu.
 Mgombea mteule kupitia CCM kata ya Misugusugu,Ramadhani Bogas akiomba kura kwa wakazi wa Misugusugu katika uzinduzi wa kampeni 

 Baadhi ya wana CCM na wakazi  wa Misugusugu wakicheza katika uzinduzi wa kampeni kata ya Misugusugu,uchaguzi katika kata hiyo unarejea baada ya kutenguliwa na mahakama ya mkoa wa Pwani.
Katibu wa CCM mkoa wa Kusini Unguja, Sauda Mpambalioto, akimuombea kura mgombea mteule wa ugombea udiwani kupitia CCM, Kata ya Misugusugu Ramadhani Bogas.
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoani Pwani,Hassan Mtenga,amevitaka vyama pinzani viache kudanganya watanzania kuwa hakuna maendeleo yanayofanywa na serikali na badala yake vifanye tathmini na kwenda na data ili kupata majibu.
Aidha amesema mwenye macho aambiwi tazama ,ni ukweli unaoonekana kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia CCM inatekeleza ilani yake kwa kuleta maendeleo ya wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Misugusugu ,Mtenga alisema wakazi wa kata hiyo wasikubali kudanganyika wakati wanaiona serikali inavyochapa kazi. 
Mtenga alieleza kuwa ,wapinzani kwa sasa wamezimwa,hawana jipya ,wanatapatapa hivyo watanzania wawapuuze kwa mambo ya uzushi wanayoyaibua.

Alisema kuna kila sababu ya kuwajibu wachache wanaojaribu kuiharibia sifa serikali kwa yale inayoyafanya ili kuwakomesha wasiendelee kuipaka matope.
“WanaCCM tafuteni kura kwa umoja wenu,msijiamini kwa kutafuta kura majukwaani,kura hazipatikani kwenye majukwaa pekee ,fanyeni kazi,tumieni maarifa ,piteni nyumba kwa nyumba kupata kuipa ushindi CCM”alisema Mtenga.
Katibu huyo wa CCM mkoani hapo,akijibu hoja zinazoibuliwa kwenye kampeni zinazofanywa na Chadema katika kata hiyo, alieleza kwamba ,hali ya kiuchumi wa Tanzania unaelekea kwenye asilimia 9 kutoka nne.
Aliwataka wasiropoke kwenye majukwaa  pasipokuwa na tatwimu halisi,waache kuongea bila kuwa na data hali inayosababisha kupotosha watanzania.

Kuhusu miundombinu alifafanua kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma ni km 641 ambapo watanzania wanatembea kwenye lami,Mtwara hadi Dar es salaam km 514,Dar es salaam-Iringa km 500.1 ni lami ,Dodoma –Mwanza km 334.Mwanza -Geita kupitia Nyakanazi yenye km 644 nayo ni lami.
Mtenga alisema Tanzania lazima ijivunie kuwa na miundombinu ya barabara bora kwa kiwango cha lami ambapo kwasasa inafikia km 18,900.
Nae katibu wa CCM mkoa wa Kusini Unguja ,Sauda Mpambalioto ,alimuombea kura mgombea mteule wa ugombea udiwani kupitia CCM ,Ramadhani Bogas na kusema anafaa kuwa kiongozi na sio bora kiongozi.
Alisema upinzani haumaanishi hata penye sifa kukatolewa dosari na badala yake kwenye sifa ama maendeleo haina budi pakaungwa mkono.
Sauda alisema CCM imefanya mengi ndani ya nchi tofauti na miaka 50 iliyopita hivyo ambae haoni maendeleo hayo ana lake jambo. 
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Kibaha Mjini, Rugemalira Rutatina, aliwaasa vijana kuacha kutumika kama ngazi na watu wachache kwa maslahi yao binafsi.
Rutatina ,alisema sio wakati wa kuchanganya madalanzi na machungwa hivyo wakazi hao wachague diwani wa CCM ili kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande wake ,mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini Maulid Bundala alisema anaimani na Bogas kwani ni mtu makini na muwajibikaji.
Aliwaomba wakazi wa Misugusugu kumchagua Bogas ili kutimiza majifya matatu ikiwa ni pamoja na rais,mbunge na diwani.
Mgombea udiwani kupitia CCM katika kata hiyo,Bogas aliwaomba wakazi wa kata hiyo kumpa kura ili kushirikiana kuinua maendeleo yao.

Aliahidi kutatua kero mbalimbali zinazogusa sekta ya elimu,afya,miundombinu kwa kuzifikisha sehemu husika na kupatiwa ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages