Akihusishwa katika kesi ya rushwa, afisa mwandamizi wa Misri ajiua gerezani.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Kitaifa la Misri amejiua Jumatatu hii Januari 2, siku
moja baada ya kukamatwa kwa uchunguzi kuhusu rushwa, maafisa wa mahakama
wamesema.
Shalaby
Wael alikamatwa Jumapili alifajiri Januari 1, 2017 kwa kuhojiwa kuhusu
kesi ya hongo katika mahakama ya juu ya nchi hiyo.
Kukamatwa
kwake kunakuja siku chache baada ya Mamlaka ya Ukaguzi kwa Viongozi,
inayohusika na kupambana dhidi ya rushwa katika taasisi za umma,
kumkamata afisa wa ununuzi katika Baraza la Kitaifa, Gamal al-Labban.
Maongezi
ya simu ya Gamal al-Labban yalionyesha kuwa Chalabi "alihiriki katika
mambo kadhaa" yanayoendana na uchunguzi unaoendelea, amesema afisa wa
mahakama.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269