Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na vikundi
vya wanawake na vijana kutoka katika Jiji la Arusha kabla ya Kukabidhi
hundi za Mikopo ya robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha
2016/2017.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amefungua mafunzo ya
ujasiriamali kwa vikundi vinavyokopeshwa na kutoa mikopo kwa vikundi 85
vya wanawake na vikundi 40 vya vijana kutoka katika kata zote za Jiji la
Arusha.
Akikabidhi
hundi zenye thamani ya Sh Mil 624 kwa vikundi hivyo ikiwa ni mikopo ya
robo ya kwanza na ya pili kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Mhe. Gambo
amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli
zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la
umasikini.
“Mikopo
hii inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo
zilizopelekea mkidhi vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha
hizi zitawawezesha kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi
huku mkizingatia nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na
makundi mengine waweze kupata fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Katikati) akikabidhi hundi ya Tsh
Mil 425 kwa wawakilishi wa Wanawake Bi. Mariamu Okash(Kata ya Kati) na
Rose Charles(Kata ya Olorieni).
Aliongeza
kuwa tofauti na mikopo hii ya halmashauri baada ya kuwawezesha vijana
waendesha boda boda kwa kuwapatia Pikipiki 200 kundi litakalofuata ni
wakinamama ambao watanufaika na Fedha zitakazorejeshwa na vijana hao kwa
kupewa mitaji midogomidogo kadiri ya uhitaji.
Aidha
Rc Gambo alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji kuunda timu maalumu ya kuchunguza
utoaji wa Mikopo kwa Kipindi cha Miaka mitatu kama ilifuata taratibu,
vikundi vilivyonufaika kama ni hai na hali ya urejeshaji.
Naye
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay ambaye
alishiriki katika zoezi la utoaji mafunzo na kukabidhi hundi amesema
Kikundi ambacho hakitarejesha fedha zote za mkopo ama kuchelewesha
marejesho kwa namna yeyote ile hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata
ila wale watakaofanya vizuri katika biashara zao na kukuza mitaji
wataongezewa kiasi cha kukopa kulingana na hali ya shughuli zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo akikabidhi hundi ya Tsh Mil 199 kwa
wawakilishi wa Vijana Amos Kosani (Daraja II) na Janeth Prosper (Kata ya
Unga Ltd).
Mikopo
hiyo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na miongozo inayoelekeza
asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo ya
riba nafuu kwa vikundi vya wananwake na vijana na kwa jiji la Arusha
kiasi kinachotakiwa kutolewa ni Bil 1.2 kwa Mwaka huu wa Fedha hivyo
kiasi kilichotolewa ni kwa kipindi cha nusu mwaka.
Fedha
hizo zinatolewe kwenye Saccos au Vicoba vyenye nguvu katika Kata husika
ili kurahisisha usimamizi na urejeshaji wa mikopo hiyo. Hivyo Saccos na
Vicoba ndizo zinazokopesha vikundi vilivyoainishwa na Kamati ya
Maendeleo ya Kata (WDC) kwa riba ya asilimia 10 na wao hubaki na
asilimia 8 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na kurejesha Halmashauri
riba ya asilimia 2 tu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Eng. Gaston Gasana (kwanza kulia) akitoa
taarifa fupi ya Utoaji wa Mikopo ya Wananwake na Vijana kwa robo ya
kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 kwenye hafla ya kukabidhi
hundi za mikopo hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro(Kwanza kushoto) akimkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kukuabidhi hundi kwa vikundi
vya Wanawake na Vijana wa Jiji la Arusha.
Vikundi
vya Wanawake na Vijana kutoka Kata mbalimbali za Jiji la Arusha
wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo Pichani)
kabla ya kukabidhiwa Mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya
ndani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269