Breaking News

Your Ad Spot

Feb 15, 2017

MAELFU YA WANANCHI WAANDAMANA MEXICO DHIDI YA TRUMP

Maelfu ya wananchi wa Mexico wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City wakitaka kuheshimiwa nchi yao na wahajiri wa nchi hiyo. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia matamshi ya chuki na uhasama ya Rais Donald Trump wa Marekani na serikali yake dhidi ya wahajiri na Wamexico.
Ripoti zinasema kuwa wafanya maandamano hao ambao jana walikusanyika kwa wingi katika mji mkuu wa Mexico huku wakiwa wamebeba bendera za nchi hiyo, wametangaza kupinga mipango ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutaka kujenga ukuta wa mpakani na kuendelea kuwafukuza wahajiri wa Mexico huko Marekani. 
Maandamano ya wananchi wa Mexico dhidi ya Rais wa Marekani
Jumapili iliyopita pia maaandamano mengine kama hayo yalishuhudiwa katika miji mbalimbali ya Mexico katika kupinga siasa za Marekani dhidi ya nchi hiyo. Wafanya maandamano hao walisema kuwa wao wakiwa ni raia wa Mexico wanapasa kuitolea mwito serikali itekeleze majukumu yake na kuwalinda raia na mamlaka ya kitaifa mbele ya mashambulizi ya serikali ya Marekani

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages