.

JESHI LA IRANI LAUFANYIA MAJARIBIO YENYE MAFANIKIO MFUMO WA MAKOMBORA WA S-300

Mar 4, 2017

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeufanyia majaribio mfumo wa makombora wa S 300 wa Iran kwa operesheni iliyofanikiwa katika jangwa la katikati mwa nchi.
Majaribio ya mfumo huo yamefanyika leo kwa lengo la kuchunguza uwezo wa utendajikazi wake na yameenda sambamba na kumefyatuliwa makombora tofauti yakiwemo ya balestiki na ndege zisizokuwa na rubani. 
Brigedia Jenerali Farzad Esmaili, kamanda wa kituo cha Jeshi la Anga cha Khatamul-Anbiyaa katika jeshi la Iran ameliambia Shirika la Habari la IRNA kwamba, mfumo wa S-300 umeunganishwa na mifumo mingine ya ulinzi yenye uwezo ya taifa hili kama vile 'Mirsad" na "Talash' ili kulinda anga ya Iran.
Mfumo wa makombora ya kujihami wa S-300
Brigedia Jenerali Farzad Esmaili, amesisitiza kuwa jibu la bwabwaja za adui wa Iran ya Kiislamu litaonekana katika medani za vita na kuongeza kuwa, wataalamu wa Iran wameufanyia majaribio mfumo huo kwa msingi wa vitisho vya adui na kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kufahamu utendajikazi wa mfumo huo. 
Farzad Esmaili, kamanda wa kitengo cha anga cha Khatamul-Anbiyaa katika jeshi la Iran
Brigedia Jenerali Esmaili amesema kuwa, mbali na mfumo wa S-300, jeshi la Iran hivi karibuni litaufanyia majaribio mfumo wa Bavar 373 wa nchi hii ambao unashabihiana na ule wa S-300. Amesema kuwa, mfumo wa S-300 wa Iran ni wa kisasa zaidi ukilinganishwa na ule wa S-300 wa Russia.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช