Rais
wa awamu ya pili Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa salamu za pole katika tukio la kuaga
mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa
mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12
Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika jana katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya
Tanzania katika nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama
aliyefariki tarehe 12 Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,
tukio hilo limefanyika jana katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar
es Salaam.
Rais
wa awamu ya pili Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali
Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo limefanyika jana
katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais mstaafu Serikali ya awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho
kwa mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika
nyadhifa mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili , tukio hilo
limefanyika jana katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Mjane
wa Marehemu Sir. George Clement Kahama Mama Janet Kahama (wa pili
kushoto) akiwa na familia yake wakati wa Tukio la kumuaga mume wake
ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa
mbalimbali aliyefariki katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili , tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu
Julius Nyerere Dar es Salaam jana.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa
salamu za pole kutoka Serikalini katika tukio la kuaga mwili wa
aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa mbalimbali
Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tukio hilo limefanyika jana katika
Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdurahaman Kinana akitoa salamu za
rambirambi za Chama wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa kiongozi wa
Serikali ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi katika nyadhifa mbalimbali
Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12 Machi 2017
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika katika
Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam.
Jaji
Mstaafu Mhe.Joseph Sinde Warioba akitoa salamu za pole wakati wa kuaga
mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Serikali ya Tanzania katika nyadhifa
mbalimbali Marehemu Sir. George Clement Kahama aliyefariki tarehe 12
Machi 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam jana .
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali
imesema itaendelea kuenzi na kuheshimu mchango mkubwa katika kupigania
maendeleo na ustawi wa jamii uliofanywa na marehemu Sir George Kahama
enzi za uhai wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani
na nje ya Tanzania.
Hayo
yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nnauye alipokuwa akitoa salamu za Serikali
katika tukio la kumuaga mmoja wa waasisi wa Taifa na Waziri msataafu
marehemu Sir Gorge Kahama aliyefariki dunia Machi 12 mwaka huu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri
Nape amesema kuwa Sir George Kahama alikuwa kiongozi mahiri na
aliyetekeleza majukumu yake kwa ufasaha ambapo alikuwa miongoni mwa
viongozi walioanzisha harakati za Serikali za uendelezaji wa mji wa
Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuimarisha makao makuu ya nchi.
“Marehemu
Sir George Kahama tutamuenzi kwa kuendeleza yale mazuri aliyoyafanya
katika kuijenga nchi yetu hasa katika ustawi wa jamii na kuimarisha
uchumi wa nchi”.Alisema Waziri Nape.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdurahaman
Kinana amumueleza Sir George Kahama kama kiongozi mahiri katika Chama
aliyependa maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla katika weledi wa
hali ya juu na alikuwa mchapakazi.
“Sir
George Kahama alikuwa mtumishi na kiongozi aliyetukuka ametuachia
hamasa kubwa ya kuwa viongozi bora zaidi na wenye mapenzi na Taifa letu
katika kuleta maendeleo.”Alisema Ndugu Kinana.
Marehemu
Sir George Kahama amekuwa Waziri na Kiongozi kabla na Baada ya Uhuru
wa Tanzania Bara kuanzia awamu ya kwanza hadi ya tatu ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amezikwa Jijini Dar es Salaam jana
na ameacha Mjane na Watoto.
Salaam nyingi za rambi-rambi kwa familia ya Sir George Kahama. May Sir George Kahama Rest in Peace.
ReplyDelete