Na Magreth Magosso,Kigoma
KAMANDA wa Polisi Mkoaa wa Kigoma Ferdinand Mtui ametoa mwito
kwa wakimbizi wanaoishi katika kambi za mkoani humo,wasalimishe silaha kwa viongozi wao kwa mujibu wa sheria,kanuni
na taratibu za Tanzania ,ili kutii sheria bila shuruti.
Akifafanua kauli hiyo mbele ya majira DCP Mtui alisema awali alitoa siku tatu kwa wakimbizi
wasalimishe silaha kwa mujibu wa sheria mtambukwa kwa lengo la kupunguza
utunzaji wa silaha kinyume cha sheria,ambazo hutumika katika matukio ya kihalifu
mkoani humo.
Alisema kupitia
mkakati waliouweka na viongozi wa wakimbizi wakiwemo sungusungu na viongozi wa
kambi za mtendeli,nduta na nyarugusu juu
ya msako endelevu wa kubaini wahalifu na silaha haramu unaolenga kwenye vijiji
vinavyozunguka kambi hizo na mapori makubwa yanayozunguka barabara kuu ya kigoma hadi wilayani Kakonko .
“niliagiza wakimbizi wanaomiliki silaha nyepesi za kivita na
ndogondogo wazisalimishe kwa viongozi wao,kwa nia ya kuimarisha ulinzi na
usalama kwa wananchi kutokana na kuzagaa hovyo kwa silaha hizo kinyume cha
sheria ya taifa husika.
Alieleza kuwa tamko hilo lilichangia Machi,9,mwaka huu,saa
3.00 katika kambi ya nduta wilayani kibondo askari wakiwa katika doria walifanikiwa
kuipata silaha moja aina ya SMG isiyokuwa na magazine wala risasi yenye namba 66-20148294 iliyokuwa imetelekezwa katika pori
lililo karibu na kambi hiyo.
Aliongeza kwa ksuema mchakato unaendelea kuwapata wahusika
waliotelekeza silaha hiyo,ili sheria ifuate mkondo wake na kuwasihi wananchi
watoe tarifa za wahalifu ili,kukomesha matukio ya utekaji mabasi ya abiria na
mauwaji wa raia wasio na hatia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269