Breaking News

Your Ad Spot

Mar 19, 2017

PADRI WA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU AIOMBA SERIKALI IWAWAONDOLEE MZIGO WA KUWALIPIA LESENI MADAKTARI BINGWA WANAOKUJA KUWAFANYIA UPASUAJI WATOTO WA KITANZANIA

Daktari Bingwa  wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kulia) akimfanyia uchunguzi wa Kinywa na meno Shabani Jafari (9)  katika Kituo cha Watoto wenye Ulemavu cha Mlali kilichopo  Kata ya Mlali, Mkoa wa Dodoma Wilaya ya Kongwa leo, kushoto ni Daktari wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Anold Mtenga.
----------------
Na Khamisi Mussa. 
PADRI na Mkurugenzi wa Kituo cha watoto Wenye Ulemavu, Paul Shewiyo , amewashukuru Madaktari wa Chama Cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno kwa moyo wao wakujali na kujitolea kwa kuwatembelea watoto wa kituo hicho kwa kutowa Elimu ya upigaji mswaki na utunzani wa kinywa na meno, kuwachunguza na kutibu  sambamba na zawadi mbalimbali .

 Shewiyo, alisema toka Duni kuumbwa ni kwa mara ya kwanza kituo hicho kutembelewa na madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno, hivyo alipata nafasi ya kuwashukuru na kuendelea kuwawaomba wazidi kutembelea watoto hao na kuomba Jamii kusaidia kituo hicho.

Shewiyo, aliendelea kusema akiiomba Selikali kusikia kilio chao kwa kuwaondolea mzigo wa kodi wanao endelea kulipa Serikalini  ambapo kituo hicho hakina mfadhili na kinaendeshwa na watu wanaoendelea kujitolea kituoni hapo, Shewiyo, akiwaombea kwa Mungu madaktari hao  katika kuwahudumia wananchi kwa ujumla.

 Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro alisema katika kuelekea Wiki ya Kinywa na Meno ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuongoza 
matembezi ya Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno yatakayofanyika mkoani Dodoma  Machi 19 mwaka huu.

Matembezi hayo yatafanyika katika Viwanja vya Nyerere Square na kuwashirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya na wananchi wa mkoa huo Sanjari na matembezi hayo siku itakayofuata Machi 20, ambayo itakuwa ni kilele cha wiki ya Afya ya Kinywa na Meno Tanzania na Siku ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani, kutakuwa na uchunguzi wa afya ya kinywa ya meno kwa wananchi bila malipo na katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene.
 Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro (aliye chuchumaa) akicheza na mtoto anaye lelewa katika Kituo cha Watoto Wenye ulemavu mara walipofika kutowa huduma kaituoni hapo leo
Watoto wenye ulemavu katika Kituo cha Watoto wenye ulemavu wakiwa katika chumba chao na mlezi katika kituo hicho

Padri na Mkurugenzi wa Kituo cha watoto Wenye Ulemavu, Paul Shewiyo katika picha ya pamoja na madaktari hao (wa tatu kushoto) wa kwanza kushoto ni Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dkt. Lorna Carneiro wa watu kulia ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Profesa Bakari Lemmariti onDaktariwa Kinywa na wakwanza kulia ni Naibu Mkurugenzi na Mhasibu wa Kituo hicho, Paschal Diwi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages