Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Nicholas Ralph akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuunga mkono
jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi
na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja
mbalimbali. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Ralph akielezea jinsi uongozi ulivopanga mikakati ya kuboresha kampuni zilizopo na kuanzisha nyinginezo nchini na nje ya nchi.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
KAMPUNI
ya Quality Group Limited (QGL), imesema inaunga mkono jitihada za Rais
John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za
kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo
Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam jana Machi 15, 2017, Afisa Mtendaji
Mkuu wa QGL, Nicholas Ralph alisema katika kuunga mkono vita dhidi ya
ufisadi wameanzisha mfumo unaotambua na kudhibiti uhalifu huo kwenye
taasisi (e-Governance).
Alisema
mfumo huo wa utambuzi na udhibiti unapaswa kuwepo katika idara zote za
Serikali kwani una utija ni salama zaidi hasa katika kuelekea katika
Tanzania ya maendeleo endelevu.
Ralph
alisema QGL imewekeza katika sekta mbalimbali kama afya ambapo
wanatarajia kujenga vituo 4,000 vya afya nchini kote pamoja na vioski
vya kutoa afya ili kuendana na teknolojia ya sasa na kurahisisha kila
mwananchi anapata huduma bora ya afya.
Alisema
pia wamekubaliana na kampuni kutoka nchini Urusi ili kusambaza vifaa
tiba na kampuni nyingine kutoka Marekani itatoa huduma ya ndege katika
huduma ya dharura.
“Pia
kampuni ya QGL imeingia makubaliano na kampuni kutoka nchini Ireland
kujenga na kuwekea uongozi katika utawala ambapo itasaidia kuongeza
teknolojia kwa kampuni
za ndani,” alisema.
za ndani,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema kampuni ya QGL imekuwa ikisadia wavuvi katika Kanda ya
Ziwa kwa kuwapatia vitendea kazi na matibabu, kusaidia elimu na pia
ilisaidia mapambano ya ugonjwa wa Ebola.
Alisema
kampuni yao imefanikiwa kuongeza ajira, mafunzo, kukuza uchumi ili
kuhakikisha inaunga mkono mpango wa maendeleo wa Serikali wa 2025.
Ralph
alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa viongozi na waajiriwa vijana
kupitia program ya Moreh Derech ambayo imekuwa na mafanikio makubwa.
Aidha,
alisema katika kuhakikisha kuwa wanapanua ushirikiano na taasisi za
kimataifa wamesaini makubaliano na Kampuni ya Solanika International
Tractors Limited ya India ambao watakuwa wanaingiza matrekta 1,000 kwa
mwaka hivyo kuongeza ajira 1,200 ifikapo mwaka
2018.
2018.
“Pia
tumesaini barua katika miradi ya madini ambapo tunarajia kuuzungumzia
vizuri pindi hatua zote zikiwa zimekamilika,” alisema.
Halikadhalika
alisema wamewekeza katika viwanda vya sukari na maziwa ambapo wananchi
wengi wa Kitanzania ndio watafaidika kwa kuuza bidhaa husika katika
viwanda hivyo vyenye teknolojia ya kisasa na uongozi kutoka Israel,
Ulaya na Afrika Kusini.
Ralph
alisema QGL imekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo inashirikiana na
kampuni kubwa duniani kama General Motors (GM), Honda, Isuzu,
Bridgestone na Chevrolet.
Alisema
kutokana na ushirikiano huo QGL imeajiri zaidi ya watu 667,300 na
kupata faida ya dola za Marekani bilioni 348.6 hayo yakichangiwa na
uwajibikaji, uwazi, uaminifu na mafanikio.
Alisema mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa ni sehemu sahihi ya kuchochea maendeleo ya nchi na wananchi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269