Daktariwa
Kinywa na Meno Hospitali ya Sinza Dar es Salaam, Idd Khery akimfanyia
matibabu ya Kinywa na Meno mwanafunzi wa Darasa la 3 Shule ya Msingi
Jumuishi Buhangija, Rajabu Yahaya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga leo kuelekea Wiki ya Kinywa na Meno ambapo watoto 53 jana na
leo wamepatiwa huduma hiyo bila malipo, (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Daktari
wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya (wa pili kulia) akifunga
Wiki ya Kinywa na Meno Mkoani humo katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi
Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga leo, kuanzia kushoto ni Dkt.
Anold Gemoniani kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Mwalimu wa Chuo
Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Profesa Bakari
Lembariti ,Daktari Bingwa wa Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba
Madjapa na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA),
Dkt. Lorna Carneiro
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro (wa pili kushoto) akimtambulisha Dkt, Arnold Mtenga
wakwanza kushoto kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,
Mwanamsiu Dossi (kulia) mara alipoongozana na ujumbe wake kwa lengo la
kumuaga baada ya kumaliza matibabu katika Kituo cha watoto Buhangija, wa
tatu kushoto ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya
Kaimu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi (kushoto) ambapo
kaimu Mkurugenzi huyo alisema, napenda kuwashukuru katika kuja kusaidia
kutowa huduma hiyo kwa miaka 3 mfululizo na akasema, nawaomba kujipanga
tena kurudi ili kutowa elimu kwa wakubua na ninaona kwa sasa
kunamaboresho makubwa yamefanyikakwa watoto wetu na lengo hasa ni kusiwe
na matatizo ya meno kwa watoto hao nawaomba mjekila mwaka natutazidi
kuwapa ushirikiano kwani watoto hao niwakwetu sote, kama mnavyojuwa
Serikali inawadau tutashirikia nao na kama kunapahala tulikosea
mtusamehe na mwisho niisiwachoshe sana niwatakie safari njema ya
kuelekea Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi katika picha ya pamoja na madaktari
Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro (wa tatu kulia) akizungumza na walimu wa Shule ya Jumuishi Buhangija (pichani hawapo) aliwashukuru kwa mapokezi yao na kutowa wito kwa walimu kuzidi kuwa karibu na watoto hao kwani niwatoto wetu na pamoja na mafanikio makubwa ya elimu ya upigaji mswaki kwa watoto hao niwakati wa kuzidi kuwanao karibu, alisema, Carneiro , tunaondoka Buhangija tukiwa tumeona mabadiliko makubwa ya mwaka wa kwanza , wapili na watatu tukiwa na furaha ya watoto kutambua umuhimu wa kutunza kinywa na meno yao, mwisho nawatakia kila la heri katika kusaidiana kuwalea watoto hao kwa kushirikiana kwa pamoja
Daktari
wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya akizungumza na mwanafunzi wa
Shule ya Awali ya Buhangija Mkoani Shnyanga, Mck Machia kushoto na
kulia ni mwanafunzi wa shule hiyo, Pasi Mugisi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269