Breaking News

Your Ad Spot

Mar 20, 2017

RAIS WA BENKI YA DUNIA AWASILI TANZANIA, KUPIGA KAZI NA RAIS DK. MAGUFULI, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO,

Dar es Salaam, Tanzania
Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dk. Jim Yong Kim, jana, amewasili nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo leo, Jumatatu, Machi 20 2017, atakutana na Rais Dk. John Magufuli, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Rais huyo wa Benki ya Dunia, alipokewa na mwenyeji wake,  Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Isdor Mpango. 

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawsiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango imesema, mazungumzoya Dk. Jim Yong Kim, na Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo  pamoja na mambo mengine yatahusu watazungumzia utekelezaji wa miradi mikubwa inayotarajiwa kufanyika kwa ufadhili wa Benki ya Duniana kisha watashiriki uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara za Juu katika eneo la Ubungo (Ubungo Interchange) jijini Dar es salaam.

Aidha, Rais Magufuli na mgeni wake watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba mitatu,  wa kwanza ukiwa ni Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri Jijini Dar es Salaam ikiwemo awamu ya tatu na ya nne ya mradi wa mabasi yaendayo haraka-DART, pamoja na ujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Ubungo (Dar es Salaam Urban Transport Project (DUTP); 

Mkataba wa pili utakuwa ni kuanza kwa Awamu ya pili ya mradi wa Uboreshaji wa Upatikanaji wa Maji safi na uboreshaji wa miundombinu ya maji taka (Water and Sanitation Project) huku mkataba wa tatu ukiwa ni wa Uboreshaji wa Miundombinu na Huduma za msingi katika baadhi ya miji (Tanzania Strategic Cities Project).

Wakati wa ziara hiyo, Dk. Kim atapata pia fursa ya kutembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Manispaa ya Ilala, ambayo ni moja ya Shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha ubora wa elimu ya msingi unaofadhiliwa ma Benki hiyo
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais huyo wa Benki ya Dunia kuitembelea nchi ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages