.

WAFANYAKAZI WANAWAKE WA BARCLAYS TANZANIA WASHEREHEKEA MAFANIKIO YAO

Mar 11, 2017

 Mkuu wa Mafunzo,  Uongozi na Usimamizi wa Talanta wa Benki ya Barclays Tanzania, Veronica Muumba (wa pili kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Fatma Karume (wa pili kulia), wakikata keki kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani katika hafla waliyoiandaa jijini Dar es Salaam jana. Wanaongalia kutoka kushoto ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo, Elizabeth Willilo, Faith Majiwa, Flavian Siweya na Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania Abdi Mohamed akizungumza katika hafla hiyo.
 Mjumbe wa Bodi ya Barclays, Fatma Karume akitoa ushuhuda wake ambapo pia alitoa changamoto kwa wafanyakazi wanawake wa benki hiyo kujiamini ili waweze kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi.

 Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Elizabeth Willilo, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Barclays Tanzania, Hellen Siria akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Benki ya Barclays jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya Barclays Tanzania wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

 Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wenzao wakieleza siri ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi za kila siku.

 Wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania wakimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu katika benki hiyo, Jane Mbwilo alipokuwa akitoa ushuhuda wake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania wakifurahia keki kuadhimisha siku ya wanawake jijini Dar es Salaam jana.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª