Breaking News

Your Ad Spot

Mar 25, 2017

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AWAONDOA HOFU WANACHAMA WA PPF KUFUATIA UAMUZI WAKE WA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake ya kufunga Mkutano wa 26 wa Wamachama na Wadau wa PPF kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha, (AICC), jijini humo jana Machi 24, 2017. Kauli mbiu ya Mkutano huo ilikuwa, “Tanzania ya Viwanda; Umuhimu na Wajibu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii”.
Katika hotuba yake pamoja na mambo mengine, Waziri alisema"Naomba niwatoe hofu Wanachama wa PPF, kuhusu uamuzi wa Mfuko kuwekeza kwenye viwanda, kwani uamuzi huu ni sahihi kwa sasa, ikizingatiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano wa kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia kwenye uwekezaji wa viwanda, lakini pia Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wa kujenga uchumi wa viwanda." Alitoa hakikisho Waziri Mhagama.
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw.William Erio, akionyesha furaha yake kufuatia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika mkutano huo ambapo alisema, jumla ya washiriki 800 walihudhuria mkutano huo na hivyo Mfuko umefanikiwa kukuza uelewa wa Wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya uwekezaji katika viwanda ambao Mifuko ya Hifadhi ya Jamii imeanza kuifanya ikiwa ni utekelezaji wa Mpango wa pili wa Maendeleo ya Taifa wa miaka 5, (2016/17-2020/21 na pia kwa madhumuni ya kuongeza mapato yatokanayo na uwekezaji na kupanua wigo wa kuandikisha wanachama kutokana na ajira zitakazoongezeka.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa, akizungumza kwenye mkutano huo. Yeye alisema Jeshi la Magereza limeamua kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo PPF na NSSF katika kutekeleza mipango ya serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, ambapo jeshi hilo kwa kushirikiana na PPF, wanafanya uwekezaji mkubwa katika kiwanda cha viatu kule gereza la Karanga mkoani Kilimanjaro na kwenye kiwanda cha sukari kwenye shamba la Mbigiri mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irine Isaka, akifuatilia kwa makini mkutano huo

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeingia siku ya pili naya mwisho jana Machi 24, 2017.



Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi, kilichoko mkoani Morogoro Nicander Kileo, akitoa mada juu ya uwekezaji wa kiwanda hicho ambacho kitamilikiwa kwa ubia baina ya Mifuko ya PPF na NSSF wakati wa mkutano wa 26 wa Wanachama na Wadau wa PPF ambao umeingia siku ya pili naya  mwisho jana Machi 24, 2017.

Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkulazi huko mkoani Morogoro, Bi.Radhia Tambwe akitoa mada kuhusu uwekezaji huo ambao unafanywa kwa ubia na Mifuko ya PPF na NSSF.

Mchokoza mada ya uwekezaji katika viwanda, Profesa Humphrey Moshi akizungumza.



Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Fabian  Daqqaro, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kulia), akiteta jambo na Mwenyekiti wa kipindi ndani ya mkutano huo, ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bi.Amelye Nyembe

Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SSRA, Bi. Sara Kibonde Msika, akifuatilia mkutano huo
 Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Msemwa, akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiendelea
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, akifurahia jambo
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, Bw. Meshack Bandawe, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uwekezaji na Mifuko hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo, (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw.Gabriel Fabian  Daqqaro.
 Waziri Mhe. Jenista Mhagama
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, (PAC), Mhe.Naghenjwa Kaboyoka, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa kikao, Mhe.Amelya Nyembe, akizungumza


Wafanyakazi wa PPF wakipoz kwa picha wakati. Wafanyakazi hao ni sehemu ya kamati ya maandalizi ya mkutano huo.


 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, akisikilzia kwa makini watoa mada
 Washiriki wakiimba wimbo wa Taifa
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitoelwa

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages