Breaking News

Your Ad Spot

May 3, 2017

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA IRINGA, MSAMBATAVANGU APATA DHAMANA

Iringa, Tanzania
MAHAKAMA  ya Hakimu Mfawidhi mkoa  wa  Iringa  imemwachia  kwa dhamana aliyekuwa  Mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa  Dk. Jesca Msambatavangu (41), aliyeshitakiwa kwa  kesi jinai namba 65 ya mwaka  2017.

Akisoma shitaka  jana,  mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Iringa Mwanasheria  upande  wa Jamhuri Alex  Mwita  alisema  kuwa Msambatavangu anadaiwa kumshambulia Neema Nyongole mkazi  wa Kibwabwa  katika Manispaa ya  Iringa Februari 17 mwaka huu  katika  eneo la Kibwabwa tukio ambalo ni kinyume na  kifungu  cha  seria kanuni ya  adhabu sura namba 16 marejeo  mwaka 2002.

Alisema upalelezi  wa  kesi hiyo  unaendelea na kutokana na  shitaka hilo upande wa  Jamhuri  hauna pingamizi ya  dhamana kwa  mshitakiwa.

Dk. Msambatavangu  alikana kuhusika na tuhuma hizo huku  hakimu anayesikiliza  kesi hiyo David Ngunyale akisema kuwa  dhamana kwa  mshitakiwa  ipo  wazi na  kumtaka kutimiza masharti  ya  dhamana ya kuwa na  wadhamini  wawili  waamini  ambao  kila mmoja atasaini dhamana ya sh. milioni moja.

Idadi ya  wadhamini waliofika mahakamani  hapo  waliweza kutimiza masharti hayo na  hivyo  kufanikiwa kutoka kwa  dhamana  hadi kesi  hiyo  itakakapo tajwa  tena mahakamani  hapo June 1 mwaka huu.

Dk. Msambatavangu  anayetetewa na mawakili  wawili  Alfred Mwakingwe na Jackson Chaula alifikishwa mahakamani hapo  mda wa saa 4: 8  asubuhi kwa  gari  la Polisi la aina ya Toyota Land Cruiser akiwa amekaa kiti cha  mbele  huku  nyuma kukiwa na ulinzi  mkali  wa askari  wa  kikosi cha FFU na  kuingizwa mahabusu ya mahakama   kwa  muda kabla ya  kufikishwa mahakamani.

Idadi   kubwa ya  wananchi walifika katika mahakama  hiyo  kusikiliza kesi hiyo,  wakiwemo viongozi wa Chama  cha Demokrasia na maendeleo  (Chadema)  walioongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wa  wilaya  Frank Nyalusi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe, Naibu  Meya  wake, huku zaidi ya watu sita  wakiwa na barua  za  dhamana na muda  wote  akiwa mahakamani  hapo Dk. Msambatavangu  alionyesha kuwa mwenye sura  ya furaha .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages