.

CHADEMA YAWARUDISHA TENA WENJE NA MASHA KUWANIA UBUNGE AFRIKA MASHARIKI

May 3, 2017

NA MWANDISHI WETU
Baada ya kushindwa kukidhi vigezo katika hatua ya kwanza, Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) sasa imewateua wanachama wake sita kwenda kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa kupigiwa kura na Bunge la Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana usiku na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema Tumaini Makene walioteuliwa ni pamoja na Ezekiel Wenje na Lawrence Masha, na walioongezeka kufikisha idadi ya wagombea sita, ni Profesa Abdalla Safari, Salum Mwalimu, Josephine Lemoyan na Pamela Massay.

Taarifa imesem, wagombea hao, wamepatikana katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichofanyika jana mjini Zanzibar na kuazimia kuwateua wanachama wao hao kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA)".

Ofisa habari wa Chadema,Tumaini Makene amesema baadhi ya mambo walioteuliwa watayakamilisha katika hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa taratibu na Kanuni za Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Awali Wenje na Masha waliteuliwa na Chadema kuwania Ubunge wa EALA, lakini wakapigwa kikumbo, kutokana na kukosa kura za kutosha katika uchaguzi wa kuwapata wabunge wa bunge la EALA, uliofanywa na Wabunge wa Bunge la Tanzania hivi karibuni mjini Dodoma.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช