.

DK. SHEIN AJIONEA UHARIBIFU NA MAAFA YALIYOSABABISHWA NA MVUA ZA MASIKA HUKO PEMBA

May 16, 2017

Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, Mkoa wa Kusini Pemba Mhe, Hemed Suleiman (kushoto kwake) alitembelea Kijiji cha Makombeni  kuangalia  nyumba mbali mbali za Wananchi zilizopatwa na athari  zilizotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha kisiwani humo jana Mei 15, 2017 wakati alipofanya ziara maalum ya kikazi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) alipofika kijiji cha Gando kumfariji na kumpa pole Mzee Juma Mjaka Khamis (kulia) akiwa na Familia yake aliyepata maafa ya nyumba yake kuangukiwa na mti na kupelekea kukosa sehemu ya kuishi baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni kisiwani humo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) alipokuwa akiangalia jengo la ZSTC Mkoani Pemba ambalo ukuta wake umeanguka kutokana na kuangukiwa na mti baada ya mvua kubwa za masika zilizonyesha hivi karibuni na kusababisha uharibifu mkubwa alipofanya ziara maalum kisiwani humo Mei 15, 2017. (PICHA NA IKULU ZANZIBAR)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช