Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2017

KADA WA CCM. MAGESA ATOA 500,000 KUKIPIGA JEKI KIKUNDI CHA SANAA CHA HISIA TEMEKE


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akizungumza na wananchi walio jitokeza wakati alipokuwa akifunga tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)


  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo (kilia) wakati alipowasili katika viwanja vya Puma kata ya Sandali Dar es Salaam jana.


Sajini wa Polisi, Mrisho Athumani (wa tatu kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (kushoto) wakati alipo alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Puma kata ya Sandali Dar es Salaam jana. kuanzia kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Zuberi Kabumaye na kushoto ni Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa


 Wasanii wa kikundi cha Hisia Threater Group wakitumbuiza wakati wa kufunga tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam juzi


 Koplo wa Bendi ya Polisi Kilwa Roard, Aleni Michael (kushoto) akitumbuiza katika  tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana


 Msanii wa kikundi cha Hisia, Masta Shivo , Shangar Omary akitowa burudani ya Sarakasi wakati wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana





 Katibu wa Kikundi cha Hisia Amina Abdallah (kushoto) akimsakili mama ambaye hakupenda jina lake kutaja wakati wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana


 Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo alipokuwa akitambulisha wageni wa meza kuu


 Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo alipokuwa akizungumza jambo  wakati wa
wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana


  Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo akipungia mkono wananchi baada ya kutambulishwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo-wakati wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji  kwa mwanamke  katika viwanja vya Puma  kata ya Sandali. Dar es Salaam jana


 Wananchi wakipitia vipeperushi wakati wa tamasha hilo


 Wasanii wakikundi cha Hisia wakitowa igizo mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa







Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo akizungumza jambo










 Mgeni rasmi akijisajili katika kitabu cha kupinga ukatili kwa wanawake, kulia ni Katibu wa Kikundi cha Hisia Amina Abdallah





Khamisi Mussa

MJUMBE wa Halimashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (MNEC), amesema  wanawake wamekuwa wakihofia kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwenye familia zao kwa kuhofia ndoa zao kuvunjika.

 Magesa aliyasema jana jijini Dar es Salaam,  alipokuwa akifunga tamasha la Tunaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya mwanamke, Kata ya Sandali jijini ambapo alifafanua endapo hayo mambo yataendelea kufumbiwa macho kwenye familia akinamama  wataendelea kufanyiwa ukatili huo bila kupata msaada wa kisheria.

Aliongeza kuwa unakuta  ndugu wa mme, mme wote wanamfanyia ukatili mwanamke, ila yeye kwa kuhofia  ndoa yake anakaa kimya bila kutoa taaria kwenye vyombo vya kisheria.

“Mtakapofanyiwa ukatili wa aina yoyote ile toeni taarifa kwenye vituo polisi, Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Makanisani, Misikitini na Vituo vya Msaada wa Kisheria ili muweze kusaidiwa  kwa kupewa elimu,”

Aliitaka jamii kutumia  fursa hiyo, kwa  kufanya mabadiliko kwenye mitaa na nyumba zao kwani kufanya hivyo ukatili hautokuwepo.Aliwasisitiza wanaume kuacha ukatili huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kufanya uharifu.

Aidha amewataka  wanaume  kuwaheshima na kuwadhamini wake zao na kuacha mabavu  ndani ya familia na pia  kuwajibika kwenye familia zao.

“Wanaume tuache unyanyasaji kwa wake zetu kwani kufanya unyanyasaji huu ni uhalifu kama ulivyo uharifu mwingine, tuwaheshimu na kuwadhamini,”alisema na kuongeza

“Kuna kina baba hawawajibiki kwenye familia zao ndio maana wamama wengi wamekuwa wakijiunga kwenye vikundi mbalimbali ili waweze kujikwamua na maisha yao.Mama zangu chukueni hatua na msilee manyanyaso ya kwenye familia na tuache kutumila  mila potofu kwa kutunza siri hata unapoona jirani au mtu yeyote anafanyiwa ukatili,”alisema.

Pia aliwataka wananchi kusaidia juhudi za Rais John Magufuli za kufanya kazi kwani kufanya hivyo hata ukatili wa kijinsia hautofanyika na kwa upande wake ameamua kutoa Sh 500,000 kwa ajili ya kusaidia kuenezwa kwa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya mwanamke nchini .

Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali wilayani Temeke, Anuciatha Kayombo alisema Suala la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake si la mtu mmoja ni la wote kwa pamoja washirikiane kutoa taarifa katika vituo vya polisi.

 “Wanawake na watoto wanapigwa hadi wanaumizwa lakini watu wamekuwa wagumu kutoa taarifa katika vituo vinavyohusika ili kusaidia matatizo haya kuisha kabisa kwenye jamii ,”alisema

Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa, kampeni hiyo ambayo ilianza tangu mwezi wa pili mwaka huu ililenga kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke ili aweze kujikomboa.

Alisema tamasha hilo  liliandaliwa na kikundi cha Hisia Threatr ikishirikiana na Kituo cha  Msaada Sheria kwa Wanawake (WLAC) kwa lengo la kutokomeza ukatili jinsia kwenye jamii.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages