Breaking News

Your Ad Spot

May 18, 2017

SERIKALI KUHAMASISHA HALMASHAURI KUNUNUA DAWA ZA KUUA VILUWIVUWI VYA MBU

Na Daudi Manongi-
MAELEZO, DODOMA.
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea kuhamasisha Halmshauri  zote nchini kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dk Hamis Kigwangala  wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando Mhe.Othman Omar Haji.


“Viuadudu hivi bimeanza kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji huu unaendelea  na endapo viuadudu ivi vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini”,Alisema Mhe.Kigwangalla.


Aidha amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali ya Cuba imeendelea kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya Afya tangu mwaka 1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.


Kupitia mkataba huo Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba ambao wamekuwa wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya , Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.


Mbali na hayo amesema kuwa Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za kibingwa kwa wananchi na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika Hospitali hizo.


Aidha kwa kushirikiana na kampuni ya Labiofarm ya Cuba,Serikali imeweza kujenga kiwanda cha kutengeneza viuadudu ivyo na Serikali ya Cuba imeleta wataalamu.


Kiwanda icho cha Biotec cha kibaha kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.5 za viuatilifu vya  kuua viluilui vya mbu waenezao Malaria  kwa mwaka

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages