Breaking News

Your Ad Spot

May 8, 2017

KIJANA GIRL GUIDES APAMBANA MEXICO KUWA MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA BADALA YA KENYA

 Mmoja wa viongozi wa vijana wa Chama cha  Tanzania Girl Guides  (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa (kulia), akilakiwa na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa wa Kimataifa wa  Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam jana.
---------------------------
Na Richard Mwaikenda 
KIONGOZI wa Vijana wa Chama cha  Tanzania Girl Guides  (TGGA), Dk. Helga Mutasingwa amefanya kazi kubwa ya kuwashawishi Wananchi wa Mexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania badala Kenya.

Dk. Mutasingwa ambaye alikuwa nchini Mexico kwa mafunzo ya miezi minne ya kubadilishana uzoefu katika nyanja za utamaduni na  uongozi alitumia fursa hiyo kutangaza vivutio vya Tanzania.


Akizungumza  mara baada ya kuwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, alisema kuwa moja ya mambo yaliyompa wakati mgumu ni kuwabadilisha wamexico kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya kama wanavyofahamu wao.


Alisema Wamexico wengi kwanza wanajua Afrika ni nchi, jambo ambalo pia ilibidi awaeleze kuwa  siyo nchi bali ni bara kama yalivyo mabara mengine duniani na katika bara hilo kuna nchi nyingi na mojawapo ni Tanzania anayotokea yeye.


Alisema akiwa huko licha ya kuwafundisha kiswahili pia alitangaza vivutio vingi  vya utalii vilivyopo nchini, ambapo aliwatajia wadudu, ndege za kila aina na  wanyama mbalimbali waliomo kwenye hifadhi za Serengeti, Ngorongoro Crater na nyinginezo.


Pia aliwafundisha kuhusu utamaduni wa Tanzania zikiwemo ngoma za asili, upikaji wa vyakula vya kitanzania kama vile ndizi na pilau, mambo ambayo walifurahishwa nayo.


Dk. Mutasingwa alisema kuwa ambaye katika ziara hiyo ya mafunzo alikuwa na vijana wenzie wa Girl Guids kutoka Venezuela,  Canada, Uingereza  na Argentina alipata wasaa wa kujifunza utamaduni wa mexico na kutoka nchi hizo zingine.


Alisema kuwa alijifunza mambo mengi ikiwemo ujasiri wa kufanya kazi bila woga, siasa za mataifa mbalimbali,  mambo ambayo ameahidi kuwafundisha vijana wenzie wa TGGA hapa nchini.


Dk. Mutasingwa aliwasili nchini jana, ambapo kwenye Uwanja wa Ndege wa JNIA, alilakiwa na Katibu wa Kitaifa wa TGGA, Grace Shaba pamoja na wanachama wenzie Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi.






 Dk. Mutasingwa akiwa na Katibu wa TTA Taifa, Grace Shaba (kushoto), Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi baada ya kulakiwa akitokea Mexico
Dk. Mutasingwa akifurahia jambo na  Elieshupendo Michael na Maryrehema Kijazi.
 Dk Mutasingwa akikumbatiana kwa furaha na Maryrehema Kijazi
 Ni furaha iliyoje kukutana
  Dk. Mutasingwa akifurahi wakati akilakiwa na Elieshupendo Michael
Grce Shaba na Dk. Mutasingwa wakiwa na furaha

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages