.

UPUNGUFU WA WAUGUZI HOSPITALI YA YAIFA MUHIMBILI KUTAFUTIWA UFUMBUZI

May 20, 2017

 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na wauguzi jana mei 19. 2017 katika maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani ambayo hufanyika Mei 12, kila mwaka ampapo kitaifa yalitanyika Mkoani Singida hivi karibuni. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Baadhi ya Mamenena na Wauguzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru
  Baadhi ya Wauguzi wauguzi wakiandika jambo wakati  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru alpokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo.
Wauguzi wakifuatilia jambo wakati maadhimisho hayo

Wauguzi wakiwa katika utulivu wakisikiliza


Wauguzi wakiwa katika utulivu wakimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru alpokuwa akizungumza katika maadhimisho hayo jana mei 19, 2017


Mmoja wa muuguzi akichangia mada katika hayo
 Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Sebastian Luziga akizungumza kwenye maadhimisho hayo .
Mweka hazina Msaidizi Tanna Taifa, Josephine Lwambuka (mbele aliyevaa bluu) akisikiliza kwa umakini akiwa na wauguuzi wakati alipokuwa akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam jana Mei 19, 2017 
Mkurugenzi wa Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kulia ) akiwanyesha wauguzi hao kijarida cha shaha  ya kitambulisho cha leseni ambacho anahitajika muuguzi kuwanacho ili afanye kazi

Mgeni rami katika Maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa akiingia ukumbini

 Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Museru akipokea risala kutoka kwa Debora Bukuku baada ya kuisoma kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (kulia) akiwaongoza baadhi ya wauguzi kuuwasha mshumaa wakati wa Maadhimisho hayo
Baadhi ya Wauguzi wakiwa wamewasha mishumaa kabla ya kurudi kula kiapa wakati wa Maadhimisho hayo


Mkurugenzi wa Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa, akiwaongoza Wauguzi kurudi kula kiapo wakati wa Maadhimisho hayo
 Baadhi ya Wauguzi wakirudia kiapo kwamba wataendelea kutoa huduma kwa wagonjwa kwa kuzingatia uadilifu.

Wauguzi wakirudia kula kiapo wakati wa Maadhimisho hayo

Dalila Sharif
MKURUGENZI wa Huduma za Uguuzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa amesema wauguzi wote wanatakiwa kuwa  kitambulisho cha leseni ndio waweze kutoa  huduma  kwa wateja (wagonjwa) tofauti na hivyo kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi milion 5.

Akizungumza Dar es Salaam jana,wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi Dunia yaliyofanyika katika tawi la hospitali hiyo,alisema Agnes kuwa wauguzi wengi hufanya kazi bila kuwa na vibali vya leseni hali ambayo kinyume na sheria ya hutoaji wa huduma kwa wagonjwa.
“hivyo sheria hii itachukua mkondo wake kwa kila muuguzi ambaye ataenda kinyume kwa kutokuwa na leseni ya utoaji wa huduma  ya pratikali kwa wagonjwa na kuitumikia adhabu hii,”alisema Agnes.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo,Lawrence Museru alisema kila muuguzi huwa na kitambulisho cha kufanyia kazi kwa ajili ya kutoa huduma hiyo hivyo kama mtoaji wa huduma anapaswa kuheshimu taaluma hiyo.

“Hivyo pia nawataka wafanyakazi kutumia lugha nzuri kwa wateja wetu ambao ni wagonjwa katika kutoa maneno yanayostahiki ili kutokuwakwaza kama yanavyosemwa kwa baadhi ya wafanayakazi kutokuwa na lugha nzuri,”alisema Museru.

Pia alieeleza kuwa zipo baadhi ya changamoto kwa wafanyakazi kuhusiana na vitendea kazi na baadhi ya wafanyakazi waliondoka kutokana na kufoji vyeti.

“Hivyo Hospitali yetu imeweza kupungukiwa na baadhi ya wauguzi walioondoka wenyewe kwa kutokuwa na vyeti halali hivyo imeweza kupunguza idadi ya wauguzi na kubaki 1200 na kadhalika,”alisema Museru.

Alisema kukabiliwa na uchache katika chumba cha ICU ambayo inahitaji zaidi waguuzi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wagonjwa hao.

Aliwataka wauguzi wafanye kazi na kufata maadili ya taaluma kwa kuwa na nidhamu na tabia njema na kuwabaini wachache wanaochafua taswira ya uuguzi kwa kuwaonya bila kuwafumbia macho.

“Hivyo wauguzi mshiriki katika kuongeza mapato ili muweze kuongezewa mapato ya ndani ambayo itasaidia kulipa baadhi ya madai na kuhusu suala la sare za wauguzi tunalifanyia kazi kila muuguzi kupatiawa,”alisema Museru.

Mwisho.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª