Breaking News

Your Ad Spot

May 15, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AYAFAGILIA MASHINDANO YA MBIO YA DASANI

 Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Yusufu Singo (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa mashindano ya mbio ya Km 21 ya Dasani Marathon 2017  baada ya kuwakabidhi zawadi zao eneo la Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam leo. Mshindi wa kwanza, Augustine Sule (aliyesimama juu), Mshindi wa pili Stephano Huche (wa pili kushoto) na mshindi wa tatu Said Makula. Kushoto ni Nalaka Hettierachchi Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza iliyodhamini mashindano hayo kupitia kinywaji cha maji ya Dasani. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA-KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Na Richard Mwaikenda

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe ameyafagilia mashindano ya mbio ya Dasani Marathon 2017 yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa kupitia kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo yenye umbali wa Km 10 na  21.

Pia aliipongeza Klabu ya Dar Running Club kwa maandalizi mazuri yaliyofanikisha mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza kupitia maji ya Dasani. Kampuni hiyo imeingia mkataba wa kuyadhamini mashindano hayo kwa miaka mitano.

"Nawapongeza nyote kwa kuchukua jukumu kubwa la kufanikisha maandalizi ya mbio hizi ambayo siyo tu ni nzito bali muhimu katika mchakato mzima wa kujenga utamaduni wa kuzijali afya  zetu na ustawi wa familia zetu, uelewano uliothabiti katika kutekeleza majukumu yetu ya kifamilia na kitaifa". Alisema Mwakyembe.

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka Hettierachchi alisema wanataka mashindano hayo yawe makubwa ambapo hivi sasa wana mipango ya kuyapeleka pia katika mikoa mingine nchini.

Mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya watu 1000 kutoka maeneo mbalimbali nchini, yalianzia na kuishia Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay na kupita barabara mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Ali Hassan Mwinyi.

Aliyeibuka kidedea katika mbio za wanaume za umbali  wa Km 21 ni Augustine Sule, wa pili akiwa Stephano Huche na Said Makula aliyeshika nafasi ya tatu.

Kwa upande wa Wanawake aliyeibuka mshindi ni Jacquline Sakilu, wa pili akiwa  Noela Remmy na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Antery John.

Kwa mbio za umbali wa Km 10, mshindi kwa upande wa wanaume alikuwa Sylvester Seleman, wa pili akiwa  Daniel Sinda na Paul Pascal alishika nafasi ya tatu.Mshindi wa kwanza kwa wanawake alikuwa May Naari, wa pili akiwa Sara Hitis na Asia Seleman aliyetwaa nafasi ya tatu.

Kwa upande wa walemavu aliyeshinda ni Shukuru Khalfan, wa pili alikuwa Mathias John na Jonis Stephano alishika nafasi ya tatu.

Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 21 kwa upande wa wanaume na wanawake kila mmoja alikabidhiwa sh. mil 1, wa pili sh. 750,000 na wa tatu sh. 600,000.
 Baadhi ya washiriki wakimalizia mbio zao katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
 Washiriki wakivishwa medali baada ya kumaliza kukimbia katika mashindano hayo
 Elizabeth wa NMB Bank akivishwa medali baada ya kumaliza mbio hizo
 ni mbio kwa kwenda mbele
 Mshiriki akiangalia muda alioutumia kukimbia. Kushoto ni Mwanariadha nguli wa zamani Juma Ikangaa
 Juma Ikangaa akiwavisha medali washiriki wa mbio hizo
 Mtoto akiwa miongoni mwa wakimbiaji
 Wakimalizia kukimbia

 Timu ya NMB Bank iliyoshiriki katika mashindano hayo
 Wakifurahia kumaliza mbio
 Wakiendelea na mazoezi baada ya mashindano
 Juma Ikangaa akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mbio za wanawake umbali wa Km 10, Mary Naari
 Mshindi wa kwanza wa mbio za Km 10 wanaume,  Sylvester Simon akikabidhiwa zawadi na Juma Ikangaa

 Dorothy Kipeja wa Dar Running Club waandaji wa mashindano hayo, akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi wa Km 21
 Mshindi wa kwanza wa mbio za umbali wa Km 21, Augustine Sule akipongezwa na Juma Ikangaa alipokabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo (wa pili kulia)
 Mshindi wa kwanza kwa upande wa walemavu  Shukuru Khalfan (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Michezo, Yusufu Singo pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza, Nalaka.
 Nahodha wa timu ya riadha ya Radio EFM, Maulidi Kitenge akiwapongeza waandaji wa mashindano hayo baada ya timu hiyo kushiriki ipasavyo.
Mtoto aliyeshiriki na kumaliza vizuri mbio hizo, akizawadiwa soda

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages