.

KIJANA AKAMATWA AKITAKA KUPITISHA SIMU KUPITIA CHAKULA GEREZA LA KEKO

Jun 19, 2017

KEKO, DAR ES SALAAM
Kijana mmoja amekamatwa leo akijaribu kuingiza simu tano katika Gereza la Mahabusu Keko jijini Dar es Salaam. Habari zilizopatikana, zimesema, kijana huyo alizifungasha simu hizo kwenye mapande ya nyama ambazo alitaka kuingia nazo katika Gereza hilo.

Inaelezwa kuwa alitaka kuingia na simu hizo ili wapewe wafungwa kwa ajili ya mawasiliano jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช