Breaking News

Your Ad Spot

May 31, 2017

MZEE NDESAMBURO WA CHADEMA AFARIKI DUNIA, LEO MJINI MOSHI

Aliyekuwa nguzo kubwa ya Chadema, Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo amefariki Dunia.

Mzee Ndesamburo amefariki Dunia leo Mei 31, 2017, katika hospitali ya Rufani ya KCMC mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kufuatia kifo hicho, Rais Dk. John Magufuli ametuma salam za rambirambi kwa familia, Ndugu, jamaa wa marehemu na kwa viongozi na Wanachama wa Chadema.

Taarifa iliyotolewana Ikulu Dar es Salaam, imemkariri Rais Magufuli aksema “Kwa masikitiko nimepokea taarifa za kifo cha Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini, Mzee wangu Philemon Ndesamburo kilichotokea leo tarehe 31 Mei, 2017 katika hospitali ya rufaa ya KCMC iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro, Namkumbuka Mzee Ndesamburo kwa hekima zake na uongozi wake uliozingatia siasa za kistaarabu”

Taarifa hiyo imesema, Rais Magufuli amesema alifanya kazi na Marehemu Philemon Ndesamburo wakati wote wakiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wote walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye maslai kwa wananchi wa jimbo lake la Moshi Mjini.

"Dk. Magufuli ameitaka familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo na wote waliguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu na amemuombea Marehemu apumzishwe mahali pema peponi, Amina", imemalizia taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages