Breaking News

Your Ad Spot

Jul 2, 2017

NIMEJIUZULU UDIWANI KWA TIKETI YA CHADEMA NIPATE UHURU WA KUUNGA MKONO UTENDAJI KAZI WA RAS DK. MAGUFULI

NA BASHIR NKOROMO
Diwani wa Kata ya Murriet Wilayani Arusha mjini mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chadema, Credo Kifukwe ajiuzulu nafasi yake hiyo ya Udiwani.

Akizungumza kwa simu na Msimamizi Mkuu wa Blog hii, Kifukwe (Pichani), aliyetangaza juzi hatua yake hiyo, alisema leo kwamba ameamua kujiuzulu nafasi yake ya Udiwani, baada ya dhamira yake kumsuta na kuona kwamba hawezi kufanyakazi hiyo huku akiwa ni mpinzani dhidi ya serikali ya Chama tawala.

Alisema, anaukubali kwa dhati ya moyo wake, utendaji wa Rais Dk. Joseph Magufuli na timu yake yote wakiongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, hivyo lengo la kujiuzulu kwake Udiwani kwa tiketi ya Chadema ni kutaka aweze kuunga mkono utendaji kazi wa Rais Dk. Magufuli akiwa mwananchi wa kawaida.

"Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nimeukubali kwa dhati utendaji kazi wa Rais Dk. Magufulu na timu yake, hivyo nimejiuzulu nafasi yangu ili niweze kumuunga mkono katika utendaji wake, dhamira inanisuta kuwa katika kundi linalopinga kila kitu" alisema Kifukwe.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages