Breaking News

Your Ad Spot

Oct 30, 2017

AMUUA MTOTO WAKE KWA RISASI AKIPAMBANA NA POLISI

NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
Mkazi mmoja wa Lukenge katika mkoa wa Pwani, Ally Sakalawe (43) amemuua mtoto wake na kumjeruhi Polisi baada ya kupiga risasi hivyo akikaidi kujisalimisha kwa makachero wa polisi waliokwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Blasilus Chatanda amethibitisha kutokea tukio hilo na kufafanua kuwa mtoto aliyeuawa ametambuliwa kuwa ni Mekwere Ally na akari polisi aliyejeruhiwa ni F 3438 D/CPL Leonard ambaye risasi ilimpata mkono wa kushoto.

Alifafanua, Kaimu kamanda alisema siku hiyo mkuu wa upelelezi Mkoa wa Pwani SSP Kingai akiwa na timu ya makachero walimkamata Sakalawe, akiwa na bunduki mbili aina ya gobore, risasi mark 4 na kipande kimoja cha gamba la kakakuona.

Alitaja vitu vingine kuwa ni vipande kumi vya nondo vilivyokatwa mithili ya risasi, goroli 249 za baiskeli alizokuwa anatumia kama risasi na vifurushi saba vya nyuzi ya katani alizokuwa akitumia kwenye mtutu wa bunduki kuzuia baruti.

Chatanda alielezea, katika upekuzi askari walijitambulisha kwa watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo kwa kuwataka wajisalimishe lakini Ally Sakalawe alikaidi na kuamua kufyatua risasi ovyo .

"Kati ya risasi hizo alizokuwa akifyatua alimjeruhi tumboni mtoto wake anaeitwa Mekwere Ally ambae alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kituo cha afya Chalinze, na pia alimjeruhi askari F 3438 D/CPL Leonard katika mkono wake wa kushoto na  amepatiwa matibabu katika kituo cha afya Chalinze na amesharuhusiwa " alisema Chatanda. 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages