.

WAGOMBEA JUMUIA YA WAZAZI NGAZI ZA MIKOA NA TAIFA KUCHEKECHWA WIKI IJAYO

Oct 11, 2017

NA BASHIR NKOROMO
Mbichi na mbivu za wagombea wa uongozi ngazi za mikoa na Taifa ndani ya Jumuia ya Wazazi Tanzania, zinatarajiwa kubainika baada kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo kitakachofanyika Oktoba 15 na 18, mwaka huu, katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo, amewataka wote walioomba nafasi mbalimbali ngazi za  mikoa hadi taifa kuhakikisha wanafika kwenye kikao hicho ili wapate fursa ya kujitambulisha na hatimaye kuchujwa kwa ajili ya kupatikana majina  ya wagombea yatakayofikishwa kwenye vikao vya Juu vya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya uteuzi zaidi.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Bulembo mesema nafasi zinazowaniwa  ni Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa (Bara na Zanzibar), Wawakilishi kwenye vikao vya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za Jumuiya hiyo ngazi ya wilaya, Bulembo alisema wamepokea rufani kutoka kwenye wilaya za Kinondoni, Temeke, Arusha Mjini, Songea Vijijini, Kibaha Vijijini, Bagamoyo, Chato, Mvomero, Kahama na Mtwara Mjini.

Amesema malalamiko hayo yanawahusu wagombea walioshinda nafasi mbalimbali ngazi ya wilaya ikiwemo uenyekiti na kusisitiza kuwa ikibainika wapo wagombea waliojihusisha na vitendo vya rushwa, ushindi wao utatenguliwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na waandishi wa habari, leo kwenye Makao Makuu ya Jumuia hiyo, Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu  Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Zanzibar Najma Giga. (Picha na Bashir Nkoromo)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช