Breaking News

Your Ad Spot

Nov 13, 2017

33 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA TRENI CONGO DRC

Radio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC imesema takriban watu 33 wamefariki katika ajali ya treni iliyokea usiku wa kuamkia leo katika mji wa Buyofwe Kusini mwa jimbo la Lualaba.

Taarifa kutoka Radio Okapi zinasema treni hiyo ilianguka kisha kuwaka moto.

Gavana wa jimbo la Lualaba Richard Muyej ameiambia BBC kwamba kuna ajali iliyotokea lakini hakutaja idadi ya watu waliofariki
Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages