.

RAIS DK. MAGUFULI AKIONDOKA UGANDA KUREJEA NYUMBANI BAADA YA KUHUDHURIA VIKAO VYA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC)

Feb 24, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika uwanja wa ndege wa Entebe mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC ambao ulimalizika hapo jana jijini Kampala nchini Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kijeshi kutoka Uganda kabla ya kurejea nchini. PICHA NA IKULU

MPINA APIGA FAINI SH. BILIONI 19 MELI 19 ZILIZOTOROKA BILA KUKAGULIWA

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu)akimsikiliza Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed ofisini kwake leo  wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Kisiwa Unguja. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlakaya Kusimamia  Uvuvi wa Bahari Kuu(DSFA),Hosea Gonza Mbilinyi. (Picha na John Mapepele)
 Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) na kulia kwake ni Katibu Mkuu Uvuvi Tanzania Bara Dk. Yohana Budeba wakiwa katika picha ya pamoja  na Wakurugenzi na Watendaji wa Sekta ya Uvuvi mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Kusimamia  Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) wakimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina  wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo katika ofisi ya Mamlaka hiyo Fumba katika kisiwa cha Unguja leo. (Picha na John Mapepele)
Kiongozi wa Kampuni ya  Linghang kutoka china inayoshughulika  na uendelezaji wa Utalii wa Zanzibar nchini china  Tom Zhang (katikati) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Muhamed(mwenye suti nyeupe) kushoto kwake ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga  Joelson Mpina (mwenye koti jekundu) wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya Waziri Mpina na Watendaji wake kuwasili leo Unguja kwa ziara ya kikazi. (Picha na John Mapepele)

Na John Mapepele
Serikali imezipiga faini ya Sh. bilioni moja kila moja, meli 19  meli zilizotoroka bila kukaguliwa kwa mujibu wa sheria na zimetakiwa kulipa faini hiyo ndani ya wiki mbili.

Meli hizo ambazo kwa pamoja zitalipa faini ya jumla ya sh. Bilioni 19, zimepewa adhabu hiyo na Waziri  Wa Mifungo na Uvuvi Luhaga Mpina kutokana na kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni ya kumi ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kutoripoti katika bandari Dar es Salaam, Zanzibar, Mtwara au Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutoka katika bahari kuu ya Tanzania.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika Ofisi za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari  Kuu zilizopo Fumba Kisiwani Unguja, Mpina  amesema pamoja na meli hizo kuamriwa kulipa faini ya Sh. Billioni moja kila moja zinatakiwa  kurejea katika bandari za Tanzania kwa ajili ya ukaguzi kwa kuwa leseni zao bado hazijaisha muda wake hadi sasa ili kubaini thamani halisi ya kiasi cha fedha zitakazotozwa kwa ajili ya samaki waliovuliwa bila kukusudia(Bycatch).

Aidha Mpina amesema  meli hizo zimetakiwa kuilipa Tanzania kiwango cha pesa kwa mujibu wa soko la kimataifa kutokana na kuondoka na Bycatch waliyoripoti kuwa wanayo kabla ya kutoroka.

Waziri Mpina amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba  kuiamru Mamlaka ya uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) iwaandikie notisi wahusika wa meli hizo kuwajulisha kuhusiana na maamuzi hayo pia kuwajulisha Kamisheni ya Jodari kwenye Bahari ya Hindi, (IOTC) kuhusiana na hatua zilizochukuliwa na Tanzania dhidi ya meli hizo ili isaidie kuwabaini na kuwachukulia sheria kwa mujibu wa Sheria husika. 

Aidha imeamriwa kwamba Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pia iandae barua/ andiko kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili aweze kuiandikia Barua Wizara ya Mambo ya Nje kwa lengo la kuwasiliana na Flag States (Mataifa ambayo meli hizi zimesajiliwa) ili kuwajulisha makosa yaliyotendwa na meli husika pamoja na hatua ambazo Tanzania imechukua. Amesema meli zote zilizotoroka zimesajiliwa nchini China.

Wakati huo huo Waziri Mpina amesema  meli ya Tai Hong 1 imekiuka Kifungu cha 18 cha Sheria ya uvuvi wa Bahari kuu No. 1 ya Mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007 pamoja na Kanuni ya 66 ya kanuni za uvuvi wa Bahari kuu za Mwaka 2009 na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kukutwa na mapezi ya papa yasiyoendana na miili iliyokutwa kwenye meli hiyo baada ya kukaguliwa katika bandari ya Dar es Salaam mnamo tarehe 25/01/2018-27/01/2018. 

Pia meli hii imebainika kukiuka kanuni ya 10 ikisomeka pamoja na kanuni ya 68 ya kanuni za uvuvi wa Bahari Kuu za mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016 kwa kuhaulisha mabaharia kutoka kwenye meli nyingine ambao idadi yao ilikuwa mabaharia kumi.

Aidha meli hiyo pamoja na kukutwa na makosa hayo iliondoka nchini bila kufuata taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa vifungu tajwa hapo juu.

Kutokana na makosa hayo imeamriwa na Mamlaka ya Bahari kuu (DEEP SEA FISHING AUTHORITY) kulipa jumla ya faini ya Sh. Billion moja ambapo Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu itawasilisha notisi ya adhabu hii kwa wahusika wa Meli hii ya TAI HONG 1.

Mbali na Tai Hong 1 Mpina amezitaja Meli hizo zilizopigwa faini ya Bilioni moja kila moja kuwa ni pamoja na TAI HONG NO2 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/453, TAI HONG 8 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/454, ,TAI XIANG 2 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/455, TAI XIANG 5 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/456, TAI XIANG 1 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/457, TAI XIANG 8 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/458 na TAI XIANG 9 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/459.

Nyingine ni TAI XIANG 10 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/460, TAI XIANG 7 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/461, TAI XIANG 6 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/462,  TAI HONG 6 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/463,  TAI HONG 7 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/464, XIN SHIJI 81 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/466, XIN SHIJI 82 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/467, XIN SHIJI 83 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/468, XIN SHIJI 86 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/470, XIN SHIJI 72 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/471, XIN SHIJI 76 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/472 na JIN SHENG 1 yenye  namba ya leseni TZ/DSFA/EEZ/473.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk. Yohana Budeba amewataka wawekezaji kwenye  bahari ya Tanzania kuwa waaminifu na kuzingatia masharti na taratibu za kisheria  ili nchi na wawekezaji waweze kunufaika.

“Taratibu zipo wazi ni muhimu  kuzinangatia sheria  namna nyingine tutaendelea kusimamia sheria za nchi yetu kwa faida ya sasa na vizazi vya baadaye” Alisisitiza Dkt. Budeba.

Amesema  hatua iliyochukuliwa na Serikali  ya kuzipiga faini meli hizo ni somo kwa meli nyingine na kwamba Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa yoyote atakayebainika kutenda  makosa  ya uvuvi haramu katika bahari na maziwani.

Aidha amesema Serikali ipo tayari kufanya biashara  na mtu yoyote ambaye atazingatia masharti ya nchi, na kwamba taifa linajipanga ili kuwa na makampuni yake ya TAFICO na ZAFICO yatakayoshuhulika na uvuvi ili kunufaika na raslimali za uvuvi kama ambavyo inafanyika katika nchi mbalimbali duniani.

Amesema hatua hiyo itasaidia kukuza ajira kwa wananchi, uchumi wan chi na kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki na mazao yake.

Aliwashukuru  wadau wote wanaoshiriki kwenye mapambano ya uvuvi ambapo kipekee alilishukuru shirika lisilo la kiselikali la Sea worrior kwa kutoa mchango mkubwa kwenye operesheni Jodari ambayo imefanywa  na wadau mbalimbali nchini.

UBALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA SIKUKUU YA KITAIFA NA UKOMBOZI

Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania uliandaa hafla ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Kuwait, miaka 27 ya Ukombozi na miaka 12 tangu Mfalme wa Kuwait Mheshimiwa Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah apokee uongozi wa nchi hiyo. 
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali wakiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Suzan Kolimba, Waziri mkuu mstaafu Dr.Salim Ahmed Salim, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, Naibu Waziri wa Ndani Mhandisi, Hamad Masauni pamoja na viongozi wa juu wa serikali, mabalozi wa nchi za kigeni na mashirika ya kimataifa na wataalamu wa fani mbalimbali na vyombo vya habari

theNkoromo Blog: MAGAZETI YOTE YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 24, 2018
MAFUNZO YA MADAKTARI WA KANDA YA KASKAZINI YALIYORATIBIWA NA WCF YAMALIZIKA

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, MOSHI

MADAKTARI na watoa huduma kutoka Kanda ya Kaskazini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku tano (5), ya kufanya tathmini ya mfanyaakazi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi amesema wamepata nyezo muhimu itakayowasaidia kutekeleza majukumu hayo kwa usahihi na haraka.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika mjini Moshi, Februari 23, 2018, Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre alisema, wengi wao walikuwa hawafahamu nini cha kufanya wanapomuhudumia mfanyakazi aliyepata madhara yatokanayo na kazi, ili kumfanyia tathmini kwa ajili ya kulipwa Fidia stahiki bali walitumia uwezo wao wa kawaida wa kidaktari.

“Mafunzo yametuwezesha ni jinsi gani daktari utafanya tathmini na ukadiriaji wa matatizo mbalimbali yatokanayo na kazi mbalimbali aliyopata mfanyakazi, kuelewa mgonjwa wa aina fulani anapofika kupatiwa huduma utamuhudumia kwa kutumia vigezo vilivyopo kisheria, lakini pia usahihi wa kujaza takwimu zake katika kumbukumbu za kitabibu.” Alisema.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Moshi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja

Aliupongeza Mfuko kwa kuandaa mafunzo hayo kani yatawezesha kuwepo na madaktari ambao wamepatiwa mafunzo maalum ya kufanya tathmini ili kutoa fidia inayostahili.

“Tulikotoka jamani hatukuwa na utaratibu maalum unaoeleweka kwamba ukiumia kazini unaenda kumuona nani na huyo mtu unaeenda kumuona hujui ni lini atakufidia kulingana na ulemavu ulioupata.” Alisema Bw. Masanja.

Lakini pia, aliwaasa madaktari na watoa huduma hao, kutumia elimu waliyopata ili kutoa tathmini sahihi na hatimaye mgonjwa aliyeumia aweze kupata haki stahiki na kwa haraka.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar alisema, jumla ya washiriki 66 kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga walishiriki mafunzo hayo, chini ya wataalamu wa WCF na wawezeshaji waliobobea kwenye maswala ya usalama mahala pa kazi kutoka taasisi ya Mifupa MOI.

Alisema mafunzo haya ni mundelezo wa mafunzo kama haya ambayo yamekuwa yakifanyika kwa awamu kwenye kanda mbalimbali nchini, ili kujenga mtandao wa wataalamu wa kufanya tathmini ya ulemavu uliotokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi kwa mujibu wa mkataba.

“ Idadi ya madaktari ambao wamepatiwa mafunzo haya nchi nzima hadi sasa ni 655 na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi ili wafanyakazi waweze kupata huduma kwa ukaribu lakini kwa haraka na usahihi.” Alifafanua Dkt. Abdulsalaam.

Baadhi ya Madaktari na watoa huduma za afya wakionyesha stika, watakazobandika kwenye milango ya ofisi zao ili kumrahisishia mfanyakazi anayehitaji kufanyiwa huduma ya tathmini. Stika hizo zimetolewa na WCF kwa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi yaliyomalizika Februari 23, 2018 mjini Moshi.
Katibu Tawala  Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo, Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza.
Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi wa WCF, (mbele), akiwa na washiriki
 
Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre, akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akionyesha stika hizo za utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akimkabidhi stika ya utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini, DktJosephine Rogate, kutoka Hospitali ya Mawenzi.
 Mmoja wa washiriki Dkt. Theresia Temu
 Mgeni rasmi, Katibu Tawala  Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bw. Sebastian Masanja, akimkabidhi cheti Dkt. Theresia Temu, cha ushiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo na kazi,  yaliyowaleta pamoja madaktari 66 kutoka mikoa ya Kaskazini, 


 Baadhi ya washiriki

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)


Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
 

Meneja tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini na ukadiriaji(Assessment and evaluation)

 Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar.
  Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa kuwapa uzoefu wake wa kazi katika sekta ya afya na tiba washiriki hao.
 Profesa Shao, (kulia), akiagana na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
 Profesa Shao, (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi.Laura Kunenge, katikati), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi 
 Wawezeshaji (watoa mada), kutoka kushoto, Dkt. Hussein, Dkt. Mshashu na Dkt. Mhina kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Muhimbili.
Afisa mwandamizi kutoka WCF, Dkt. Pascal Magesa,  akigawa fomu za tathmini ya mafunzo
 Picha ya kwanza ya pamoja 
Picha ya pili ya pamoja


ยช