Breaking News

Your Ad Spot

Jan 4, 2018

DK. KALEMANI AAGIZA KUPITIWA UPYA MIKATABA YA SERIKALI NA SONGAS KUHUSU GAWIWO


Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani ameitaka kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas, kupitia upya mikataba ya gawio kwa serikali ili kuhakikisha serikali inapata mgawo sawa na Kampuni hiyo na kubadilisha mfumo wa sasa ambapo serikali inapata gawiwo la faida baada ya uzalishaji.

Ni katika ziara ya Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani alipotembelea katika kampuni ya kuzalisha Umeme ya Songas, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo Dk. Kalemani akaitaka kampuni hiyo kupitia upya mikataba yao katika gawio na serikali.

Aidha Waziri Dk Kalemani amethibitisha mchango wa serikali katika uchangiaji wa uzalishaji wa sekta ya umeme sanjari na kampuni ya Songas pia lakini akakemea vikali tabia ya kutofautiana kwa mgao baina ya kampuni hiyo na Serikali.

Aidha Waziri Dk Kalemani amezitaka kampuni zote za uzalishaji nchini kuacha mara moja tabia ya kuagiza mitambo ya uzalishaji nje ya nchi na badala yake ipatikane hapahapa nchini.

Kwa upande wake Sebastian Kastuli ambaye ni Meneja Biashara wa Kampuni ya Songas ameahidi kutekeleza maagizo ya Waziri na kupitia upya mikataba yao na serikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages