Breaking News

Your Ad Spot

Jan 1, 2018

RAIS DK MAGUFULI AMTUMIA SALAM ZA RAMBIRAMBI RAIS UHURU KENYATTA WA KENYA KUFUATIA WATU 36 KUFARIKI BAADA YA BASI KUGONGANA NA LORI NCHINI HUMO

IKULU DAR ES SALAAM
"Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru  Eldoret nchini Kenya.

Msiba huu umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.

Kwa niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.

Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina".


Hizi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu katika Taarifa yake imemkariri Rais John Magufuli akisema wakati akitoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu takribani 36 baada ya basi la abiria kugongana na roli katika barabara ya Nakuru - Eldoret nchini humo leo tarehe 31 Desemba, 2017.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages