.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UDIWANI KATIKA KATA KUMI

Jan 26, 2018

NA BASHIR NKOROMO
TUME yaTaifayaUchaguzi (NEC) imetangaza majina 27 ya wagombea udiwani ambao wameteuliwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwania nafasi hizo katika kata kumi ambazo zitafanya uchaguzi mdogo Februari 17, mwakahuu kufuatia nafasi kuwa wazi katika kata hizo kutokana na baadhi ya madiwani kujiuzulu au kufarini dunia.

Taarifa iliyotolewa leo na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema katika uteuzi huo wanaume waliojitokeza  kugombea nafasi hizo ni 24 wakati wanawake ni watatu na kwamba katika uteuzi huo wagombea wa Kata nne waliteuliwa Januari 20 na wagombea wengine wa kata sita waliteuliwa Januari 24 mwakahuu.

Wagombea waliojitokeza kuwania udiwani katika kata ya Buhangaza iliyoko wilaya ya Muleba mkoani Kagera na vyama vyao ni JenithaTibihenda (CCM), Nelson Makoti (Chadema) na Grayson Aniceth (NCCR Mageuzi). 

Katika Halmashauri ya Siha iliyoko mkoani Kilimanjaro ambako kuna kata tatu zitakazofanya uchaguzi mdogo, wagombea waliojitokeza katika kata ya Gararagua ni Zakaria Lukumai (CCM) na Agness Lasway (Chadema) huku katika Kata ya Donyomuruak wagombea ni Lwite Ndossi (CCM) na Daniel Molle (Chadema) na katika kata ya Kashashi wagombea ni Suzan Natai (CCM) na Immanuel Saro (Chadema).

Mkoani Mwanza ambako kuna kata mbili, wagombea katika kata ya Kanbyelele iliyoko Halmashauri ya Misungwi ni Marco Yela (ACT Wazalendo), Daniel Makoye (CCM) na George Mhoja wa Chadema huku katika Kata ya Isamilo iliyoko wilaya ya Nyamagana wagombea wakiwa ni Nyamasiriri Marwa (CCM), John Kisyeri (Chadema), Hashim Ramadhan (CUF), Georgina Kibendegele (DP) na Ramadhani Mtorowa UDP.

Kwenye kata ya Mitunguruni iliyoko wilaya ya Singida wagombea ni Abdallah Mkoko (CCM), Manase Kijanga (Chadema) na Abdallah Kinga wa CUF na  Wagombea kata ya Madanga iliyoko wilaya ya Pangani mkoani Tanga ni Mohamed Abdallah (ACT Wazalendo), AthumanTunutu (CCM) na Swaibu Mwanyoka wa CUF.

Katika Mkoa wa Dodoma ambako pia kata mbili zitafanya uchaguzi, kwenye kata ya Manzase iliyoko wilaya ya Chamwino jimbo la Mtera wagombea ni Amos Mloha (CCM), Alex Chalo (Chadema) na Ndahani Mazengo wa CHAUMMA, wakati katika kata ya Kimagai iliyoko wilaya ya Mpwapwa mgombea wake ni Noah Lemtoa mbaye amepita bila kupingwa.

Taarifa imesema Uchaguzi huo utaenda sambamba na uchaguzi wa wabunge katika majimbo mawili ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na Siha mkoani Kilimanjaro ambapo Katika Jimbo la Kinondoni walioteuliwa na msimamiz iwa uchaguzi wa jimbo hilo kuwania ubungeni wagombea12 ambao ni Godfrey Maliza (TLP), Johnson Mwangosi (SAU) na Mwajuma Milambo kutoka UMD.

Wagombea wengine walioteuliwa ni John Mboya (Demokrasia Makini), Maulid Mtulia (CCM), Mary Mpangala (DP), Salim Mwalimu (Chadema), RajabuSalum (CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK),  Ally Omari Abdallah (ADA -Thadea) na Ashiri Kiwendu kuto kachama cha AFP  

Kuhusu uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro,  walioteuliwa ni wanne ambaoni Dk Godwin Mollel (CCM), Mdoe Azania Yambazi (SAU), Tumsifuheri Mwanry (CUF) na Elvis Christopher Mosiwa CHADEMA. Kampeni katika kata 9 na majimbo hayo mawili zinaendelea kufanyika hadi Februari 16 mwaka huu.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช