.

WAZIRI DK. MWAKYEMBE AOMBOLEZA KIFO CHA MSANII NIKI WA BONGO MOVIE

Jan 26, 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (Mb) amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Msanii maarufu wa filamu Abdul Nachona maarufu kama Niki kilichotokea jana Januari 25, 2018 jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mwakyembe (Pichani) ameeleza kuwa kifo cha Abdul kimeacha pengo kwa tasnia ya filamu na Sekta ya Sanaa hasa katika nyanja ya uigizaji ambayo marehemu alikuwa nguli.

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia ya marehemu, Uongozi wa Chemchem Arts Group, Uongozi wa Chama cha Waigizaji nchini, Wasanii na wapenzi wa filamu, ndugu, jamaa na  marafiki na kuwaombea Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Kipindi cha uhai wake marehemu Ndg. Abdul alifanya kazi na kikundi cha Chemchem Arts Group akishiriki kuigiza filamu na tamthilia mbalimbali. Marehemu Abdul atakumbukwa sana kwa uigizaji wake katika tamthilia maarufu ya Kizaazaa iliyokuwa ikirushwa na kituo cha Televisheni cha ITV.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช